Upinzani na Uzalendo....

Upinzani na Uzalendo....

Mwarabu55

Member
Joined
Jul 5, 2013
Posts
53
Reaction score
39
Kwa kipindi cha miaka miwili na ushee tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, mambo mengi yamekuwa yakijitokeza na kuulegeza upinzani hapa nchini. Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na yanayotokea kwa upande wa serikali, lakini pia yapo yanayotokea upande wa upinzani wenyewe. Tangu aingie madarakani Raisi Magufuli amejitahidi sana kukusanya mapato na kusimamia matumizi ya fedha,kuzuia rushwa na pia kurudisha nidhamu kwa watumishi wa uma.

Vimeonekana viashiria kwa upande wa wapinzani kulega, baadhi ya madiwani wakiwemo na wabunge wamehama vyama vyao na kuunga mkono jitihada za Raisi na serikali yake. Hii inapelekea kutengenezeka kwa chuki kati ya chama tawala na wapinzani wake, technical Magufuli amewazidi nguvu.

Mfumo wa wa vyama vingi tangu kuanza kwake nia ilikuwa ni kuwa na mawazo tofauti ili kusaidia kujenga nchi yetu kwa fikra tofauti na sauti from different opinions. Vyama vya upinzani visijisikie kuonewa na kuamua kupotosha wananchi ili kusaidia mripuko wa machafuko,haita kuwa jambo jema kwa taifa letu. Cha muhimu ni kusaidia serikali katika kuimarisha amani na mshikamano ndani ya taifa letu…

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom