Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,004
Ni vituko lakini ndio hali halisi..Baada ya JPM kuapishwa wapinzani kwa ujumla wao walipaza sauti ya kwamba JPM aachwe mwenyewe bila kuiniliwa na kushauriwa na maraisi wastaafu. Walianza kwa kusema 'mfumo' usimshauri raisi. Sasa baada ya Tumbua tumbua naamini mkasi umetumbua majibu hadi shina kufikia huko kwa wapinzani. Ni dhahiri wengi walikuwa ni wezi bila kubagua, kundi hili la wapinzani sasa hali imekuwa ngumu.
Tuliambiwa tatizo ni 'mfumo' sasa wanasema maraisi waliopita na mfumo ulkuwa sawa lakini JPM anabomoa 'mfumo' kiasi sasa wanapata hasara. Walichofanikiwa ni kuajiri makundi kwa makundi kutukana mitandaoni na kupitia majarida yao wamekuwa wakiandika uongo.
Kuna mambo ambayo sasa ni dhahiri;
Wapinzani hawa makanjanja ndio chanzo cha matatizo mengi tulionayo, wengi ni mawakala wa mabepari ndani na nje ya nchi.Ninaweza nikasema kwa kujiamini na hakika upinzani wa Tanzania upo kwa mujibu wa sheria lakini hauna tija. Na kwa aina ya siasa wanazofanya CCM itaendelea kutawala nchi hii kwa mitindo tofauti kwa karne nyingi zijazo. Ni nani leo anaweza kusema kinagaubaga Mbowe,Zitto,Lowassa,Mbatia,Seif na wafuasi wao wanasimamia au wanataka nini? Leo Lowassa sera yake kubwa 'nilisemwa sana, CCM walinitenga nashukuru kwa mahaba' Leo Zitto anabuni tatizo hewa na kulazimisha serikali watatue...yaani anataka serikali ichukue ushauri potofu, Leo Mbowe anatangazia umma kuwa anaenda Ghana kuchukua mbinu za ushindi kutoka kwa Nana na kujigamba ni mgeni rasmi wakati hata kwenye tukio moja rasmi la uwanjani na ikulu hakualikwa, Leo Sefu anaota kutangazwa Raisi wa Zanzibar..anasubiri UN imtangaze, Leo CUF waliosusia uchaguzi Zanzibar wajipiga vikumbo hadi kufanya propaganda kushiriki uchaguzi. Nadhani kwa ufupi umetabua ulaghai wanaoufanya, wamegeuza siasa kuwa majumba ya 'uponyaji na miujiza.
Waliopinga jana leo wanataka yafanyike tena na watu waliowapinga kuwa hawafai.
Kwa kundi hili CCM ina fursa ya kutawala karne nyingi zijazo kwa mbinu ya kuwavalisha gamba wapinzani.