Lovery
JF-Expert Member
- Aug 15, 2014
- 1,540
- 3,136
Habari zenu ndugu zangu,
Nipo katika mtihani ambao unanichanganya sana, nahitaji ushauri wa kitaalamu na hata kimawazo.
Jambo lenyewe ni hili;
Nina mke na tunaishi mbalimbali kutokana na namna ya ajira zilivyotoka, tuna mtoto mmoja.
Mzunguko wake wa hedhi ulikuwa kama ifuatavyo.
December - 18 hadi 22 ni sawa na siku 5.
January- 17 hadi 20 ni sawa na siku 4.
February-15 hadi 19 ni sawa na siku 5.
Katika miezi hii mitatu mzunguko unaonyesha 30/31/30 kama sijakosea.
Nikawa nimekutana nae kimwili February 18 hadi 19 tu, ikiwa ni siku ya 4 na 5 tokea aanze hedhi.
Jambo la kushangaza ananiambia ni mjamzito na amepima na kuhakiki hivyo.
Tafadhali inawezekanaje hali hii kutokea, maana sina imani kabisa na huu ujauzito na hii ni kutokana na tunavyoelewa siku za hatari ni 11 hadi 18.
Naombeni msaada wa elimu na ushauri ulio wazi maana sasa sipati usingizi.
Asante.