Upi Mtandao Bora wa Simu (mawasiliano)

mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,125
1,752
Natumai muwazima.
Kwa hapa Tanzania kwa sasa tuna mitandao mingi ya simu mingi ikiwa imejikita kwenye huduma ya sauti, huduma za kifedha na ingine data tuu.
Mitandao hiyo ni TTCL, TIGO, VODACOM, AIRTEL, SMART, SMILE, ZANTEL na HALOTEL.
Ni mtandao upi wenye huduma nzuri kwenye nyanja zifuatazo
1. Gharama za malipo ya Sauti (voice)
2.Gharama za malipo ya Data (Internet)
3. Huduma za kifedha (mobile financial services)
4. Huduma kwa wateja (Customer care & service)
5. Corporate service , hapa ni kwa huduma za malipo ya baada.
6. Corporate social responsibility and Public trust.
7.Mtandao upi ume enea zaidi (coverage)
8.Mtandao Upi wenye Ofa nzuri na una jali wateja.
Ni hayo tu..
 
Wote wezi! Tofauti yao ni namna ya kukuibia wengine wanang'ata wanapuliza wengine wanakomba wengine wanajifanya hawahusiki ila wanapunguza mb kila kukicha wengine wanasema spidi zao ni za mwendokasi lakini ukibugi tu utasema umechukua guta.
 
Nafurahia sana halotel uny, but nilipofika dar speed ya internet ilikuwa chini 101k/s huku kjjini inafika hadi 700k/s
 
Vodacom wana shida moja ambayo ni janga " kutoa siri za wateja wao, yaani hata kama una mchepuko wanamweleza mwenzio"
 
Mitandao yote ni mizuri na ina ubaya wake tatizo ni huduma kwa wateja,wanajeuri hao(utadhani mmeibiana bwana au mwanamke), wana dharau,kebehi(hasa jicho linavyoshushwa)
 
Natumai muwazima.
Kwa hapa Tanzania kwa sasa tuna mitandao mingi ya simu mingi ikiwa imejikita kwenye huduma ya sauti, huduma za kifedha na ingine data tuu.
Mitandao hiyo ni TTCL, TIGO, VODACOM, AIRTEL, SMART, SMILE, ZANTEL na HALOTEL.
Ni mtandao upi wenye huduma nzuri kwenye nyanja zifuatazo
1. Gharama za malipo ya Sauti (voice)
2.Gharama za malipo ya Data (Internet)
3. Huduma za kifedha (mobile financial services)
4. Huduma kwa wateja (Customer care & service)
5. Corporate service , hapa ni kwa huduma za malipo ya baada.
6. Corporate social responsibility and Public trust.
7.Mtandao upi ume enea zaidi (coverage)
8.Mtandao Upi wenye Ofa nzuri na una jali wateja.
Ni hayo tu..
TIGO ndio maana unahusishwa na mambo yote matamu duniani.
 
Kila mtandao unamapungufu yake ndio maana tunaline 3 hadi 4 kufill gaps, kwa upande wangu hakuna nnaoweza kuuita bora kushinda wengineo
 
Back
Top Bottom