Upi msimamo wa ACT juu ya uchaguzi wa marudio Zanzibar?

Magnesium

JF-Expert Member
Nov 9, 2014
317
185
Wanabodi habari ya muda huu? Kusema ukweli nimefurahishwa sana na uamuzi wa Zitto Kabwe na ule wa UKAWA wa kuweka tofauti zao pembeni kwa maslahi ya taifa. Na pia hili la andiko la Mbowe na ZZK juu ya kuacha tofauti zao na uadui na kufanya kazi ndilo linaloniongezea furaha zaidi kuona upinzani ukikomaa.

Ni hivi majuzi tumeshuhudia Chama Cha Wananchi (CUF) ambacho ni chama mwenza ndani ya umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kikitangaza kususia na kutoshiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar kutoka na sababu mbalimbali tunazozifahamu. Cuf wamefikia hatua ya kuitaka ZEC kutochapisha Majina ya wagombea wa CUF, picha wala nembo yao.

Sasa swali langu linakuja hapa, je ni upi msimamo wa ACT chini ya Zitto? Na wao wanaususia uchaguzi huu? Ama wao wanaunga mkono marudio hayo?

Ningependa kushauri ACT, kama kweli nia yao ni kuungana na UKAWA kwa maslahi ya Taifa, basi na wao watoe tamko la kutoshiriki uchaguzi huu. La si hivyo tujue moja Zitto bado hajamaanisha alichosema leo. Naomba kuwakilisha
 
Kiongozi Mkuu wa ACT-UJIJI, ameshafikisha umri mwezi wa12,unaoluhusiwa kikatiba kugombea Urais, hiyo atatuwakilisha huko ZANZIBAR, msiwe na hofu.
 
Back
Top Bottom