Upeo wa radio presenter wetu

chetuntu

R I P
Jan 10, 2011
949
109
Wanajamii leo mida ya saa nne kipindi cha watoto radio Praise Power mtangazaji kaongea yafuatayo nanukuu "wazaz hawamjui Mungu ndio mana walikimbia milipuko ya gongo la mboto na kusahau watoto/kupotezana nao." Sikumuelewa kwa kweli na akaongeza upendo wa wazaz kwa watoto umepungua sana. Binafsi sikumuelewa kabisa. I wish angekuwa miongoni mwa wana GMBOTO. Nawasilisha!
 
Mzazi una shughuli zako na mtoto anacheza na wenzie akisikia hata muungurumo wa radi utampata? Ndo tabu ya kusomea buguruni tsj miezi 3 haLafu unapewa mic...
 
Hao ndio watangazaji wetu maana kuna kipindi wanaongea utumbo mpaka unaamua kuzima hata redio, kwanza utakuta m2 mwenyewe ana D. Mbili kama rafiki ye2, kisa ana sehem ya kusemea nyie acheni tu inasikitisha
 
Wanajamii leo mida ya saa nne kipindi cha watoto radio Praise Power mtangazaji kaongea yafuatayo nanukuu "wazaz hawamjui Mungu ndio mana walikimbia milipuko ya gongo la mboto na kusahau watoto/kupotezana nao." Sikumuelewa kwa kweli na akaongeza upendo wa wazaz kwa watoto umepungua sana. Binafsi sikumuelewa kabisa. I wish angekuwa miongoni mwa wana GMBOTO. Nawasilisha!

watoto ndiyo waliowakimbia wazazi wao kwani hawawapendi
 
Acha kuropoka swala siyo kusoma buguruni tsj,hata angesoma mlimani,huo ni upeo wake mdogo,na ww huna akili ya uelewa.
 
Praise power hawana professional presenter hata siku moja kuna siku mtu alikuwa anajifanya ni great thinker anaeleza ni vipi unaweza kupata kazi ya u kurugenzi au u meneja alikuwa anasema kwanza lazima angalau uwe na kitambi, harafu uwe mrefu na ukitaka uwe unasikilizwa sana uwe mweupe alikuwa very serious. Nashangaa ilikuwa ya kwanza kati ya redio za dini ya kikristo nadhani kwa sababu wana waumini wengi hivyo yule mama mwanasiasa ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri na sijui nasikia pia ni mchungaji aliwaambia wafuasi wake waipigie kura.
 
Acha kuropoka swala siyo kusoma buguruni tsj,hata angesoma mlimani,huo ni upeo wake mdogo,na ww huna akili ya uelewa.
sasa na wewe unabisha nini? tsj miezi mitatu unaweza kupresent kweli?
 
Hivi sasa fani zote zimevamiwa,jamii imeharibika,vyuo vinatoa voda fasta,siyo journalism pekee bali hata sheria,udaktari,bishara,IT nk
kama unabisha taja fani yake nikupe mifano ya walioko sokoni wanavyofanya
 
Sasa si amepata pa kupanulia domo lake na kuropoka utumbo... Halafu waweza kuta kesha abort hata zaidi ya 10.
 
watangazaji wanakera sana, atakuwa hajui maana ya ajali, ni kosa lake na anatakiwa kuchuja mambo kabla ya kuyaropoka.
 
Hao wenye kumjua Mungu "walokole " mbona wamepoteza watoto zao??. Hizi kaz za kupeana kipendwa ni hatari sana.
 
Hao wenye kumjua Mungu "walokole " mbona wamepoteza watoto zao??. Hizi kaz za kupeana kipendwa ni hatari sana.
hao hawajui mshikemshike uliotokea.. kombora limetua mbele yako nyumba ikmekuwa kifusi na vumbi tele hujui mtoto ama baba au mama wako wapi inabaki wewe na roho yako..akili ikirudi ndo mtafutano unaanza
 
Back
Top Bottom