Upeo wa majukumu ya Wabunge jimboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upeo wa majukumu ya Wabunge jimboni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bitimkongwe, Jun 17, 2010.

 1. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Jamani mimi mwenzenu napata shida kuhusu majukumu ya Wabunge tunaowachagua kwenye majimbo yetu.

  Asilimia kubwa ya wananchi wanasema Mbunge wetu hakutufanyia hivi, mfano hakutujengea shule, barabara, hospitali, hakuleta maji na kadhalika.

  Naomba kueleweshwa jee upeo wa majukumu ya Wabunge ni upi? Yaani Mbunge afanye nini ili wananchi waridhike, na kwa kiwango gani? Na jee ikiwa lawama zote anatupiwa Mbunge, wale viongozi wengine kama Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya na Mikoa na Madiwani majukumu yao ni yepi?

  Jee Wabunge huwa wanapewa Terms of Reference (Hadidu Rejea) pale wanapoapishwa?

  Nitashukuru kama mutaweza kufafanua hili ili niweze kufanya assessment yangu.
   
 2. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Ki-nadhalia, Bunge ni kikao cha wananchi na watendaji wa serikari. Wananchi wanawakilishwa na wabunge maana haiwezekani wote kuingia ndani ya jengo hilo. Wananchi wanaeleza matatizo yao na Serikali inaeleza mbinu ya kuyatatua matatizo hayo.

  Kama wewe ni msomaji wa thread za JF, kuna sehemu nimeeleza juu ya wale wanaodai Mh. Selelii hajawafanyia kitu wana Nzega, eti tu hawaoni shule, hospitali, barabara, n.k. Vikijengwa. Nikasema hiyo siyo kazi ya Mbunge.

  Mbunge akisha wasilisha matatizo ya jimboni, inatosha. Kutotatuliwa kwa matatizo hayo ni tatizo au uzembe wa serikali. Serikali ya CCM.

  Kwa upande mwingine wabunge wenyewe wanajitakia matatizo kwa kujidai wana uwezo wa kuleta maendeleo jimboni. Ni majigambo ambayo yana lengo la kushawishi wapiga kura. Ndo maana wanaenda mbali hata kutaja uhusiano wao na Rais, au eti wanajulikana sana, wametumwa kuleta maendeleo, nk.

  Lakini kumbuka pia kwamba kwa nchi kama yetu ambayo ni omba omba, uwezo wa kuomba pia ni sifa ya mtu kuwa Rais au kiongozi. Hivyo unaweza kujieleza kwamba mimi ni omba omba mzuri, nichagueni.

  Na kama kweli sifa hiyo ni yako unaweza ukaomba hata bila kuihusisha serikali na ukapata msaada wa kuwasaidia wananchi wa jimbo lako. Kuna wabunge kama Slaa nimesikia wakisifiwa bungeni kwa miradi ya maji jimboni ambayo serikali hata haihusiki. Kumbuka lile sakata la mkuu mstaafu Sumaye, kung’oa mabomba ya maji jimboni.
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Asante Mchunguzi kwa ufafanuzi huo. Unajua kuna gazeti moja la kila wiki ambalo hutoa makala mbali mbali za kuwakandia Wabunge, na hasa wale ambao huwa hawawapendi. Eti huwa wanauliza wananchi halafu wananchi wanajibu kwamba hawakufanyiwa lo lote na Mbunge wao. Vile vile eti wanahoji kwa nini Wabunge wao wanatetea ufisadi na sio masuala ya jimboni kwao.

  Ndio maana nikaona bora niulizie hili suala kwa sababu ni kweli wajib wa Mbunge kutetea jimbo lake, lakini jee kwa masuala ya kitaifa (rushwa, ufisadi) ni nani anawajibika kuyaulizia? jee hawa wananchi hawaoni uhusiano baina ya rushwa na ufisadi na maendeleo ya jimboni kwao?
   
 4. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,650
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa ufafanuzi mzuri.
  Kwa kifupi ni muwakilishi wa wananchi katika baraza kuu la kutunga sheria na kuisimamia serikali.
  Ni wajibu wa serikali kukusanya kodi na kutumia raslimali nyingine za uma kuwaletea wananchi maendeleo na wabunge wanawajibika kuhakikisha kwamba serikali inawajibika vizuri na kama kuna mapungufu yanarekebishwa.(system of checks and balances).
  Jamii imepotoshwa mpaka imefikia wakati mbunge anajidai kwa kujenga miradi kwa pesa zake au ufadhili ambapo kimsingi kusaidia jamii siyo lazima uwe mbunge.
  Watu wenye pesa zao ambao wangependa kusaidia jamii wanaweza kabisa kusaidia bila kuwa wabunge na michango yao ikathaminiwa zaidi.
  Miradi inayofadhiliwa binafsi na ubunge havina uhusiano wa moja kwa moja.

  By the way, MchunguZI chunguza bolded words above!, Ahsante.
   
 5. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Kwa kawaida Wabunge wanatakiwa wawe na nguvu ya ‘kuitia adabu serikali’ ikimaanisha pale ambapo haikufanya vizuri inalazimishwa na ikibidi ijiuzuru kama ulivyosikia Japan hivi karibuni.

  Ukiliangalia Bunge letu limekuwa ni butu, nadhani kwa sababu nyingi mojawapo ikiwa ni nguvu ya chama na hasa kwa upande wa CCM. Chama kinaweza kikaamua kuondoa jina lako ktk uchaguzi bila kujali upendo wa wapiga kura wako. Ina maana Wabunge wa CCM lazima wajikombe kwa chama na bahati mbaya chama chenyewe kilizoea utakatifu kwamba hakikosei.

  Bungeni Serikali ina nguvu inafanya inavyotaka wakisaidiwa na spika ambaye ni kama anahakikisha analinda aina ya maswali ya wabunge lakini halindi aina ya majibu ya serikali. Wanajibu watakavyo. Msuya akiwa waziri akiwahi kusema hajiuzuru mpaka rais amfukuze (Jeuri hiyo).

  Pamoja na wabunge wote kutetea majimbo yao lazima waangalie ubovu wa serikali. Tatizo ni wachache wanaodiriki kusema bila kujali chama kitasema nini. Kundi kubwa lililo dhaifu limeamua kuwachukia na sasa wanahangaika kuwapiga vita wasirudi Bungeni kwa kutumia vigezo dhaifu kama hivyo. Kwamba eti hajafanya lolote jimboni.

  Ukiangalia kuna sabotage. Kwamba unajidai kuwakosoa hivyo wanaamua kulitelekeza jimbo bila sababu. Yaani eti hiyo inayoitwa serikali inaamua kutelekeza wananchi wa jimbo ili wannchi wamuchukie mbunge.

  Majimbo yoote yaliyo nyuma ki-maendeleo, ni kosa la serikali yenyewe. Na siyo Mbunge.
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kwa asilimia 50%. Ni kweli kuwa mmbunge ni mwakilishii wa watu wa jimbo lake. Kwa hiyo turudi kwenye basics. Kama wananchi wana maombi/kero/shida/matatizo na huduma zinazotolewa na serikali...ni SHARTI wapitie kwa mmbunge wao. Na hivyo...sifa kuu ya mmbunge ni kuweza kuwakilisha hayo maombi serikalini na KUHAKIKISHA yanafanyiwa kazi! Sasa hapo ndo inategemea na umakini, ujuzi na uweza wake katika kazi. Kwa mfano...kkama unaona huna nguvu unaweza kujiunga na wabunge wengine wenye matatizo kama yako na ku-lobby serikali iwasikilize. Si unajua mambo ya scratch my back and i scratch yours. Hii ndo siasi! Kwa hiyo mmbunge anaposhindwa kuleta hospitali(huduma za afya), polisi (ulinzi wa mali za watu), elimu...basi ameshindwa kazi yake! SIMPLE and CLEAR na HAFAI KUWAWAKILISHA HAO WANANCHI! Tatizo sisi tumezoea under-par, yani kiwango cha chini!
   
 7. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Unajua Serikali inapanga mipango yake ya maendeleo kwa kutegemea wataalamu wake na siyo kutegemea wabunge. Ndo maana wakija Bungeni, Serikali huja na mipango yake tayari. Haiji bugeni kusaidiwa kupanga. Inakuja kwa mbwembwe kuonyesha jinsi inavyowajali wananchi na kuomba waikubali.

  Ikifika Bungeni, Wabunge kama wawakilishi wa wananchi wanaiangalia mipango hiyo kama ina manufaa na kuanza kuikosoa ili ilete manufaa kwa wananchi kama wanavyotaka wao (wananchi). Kwa umoja wao kama siyo hizi bla-bla zetu wanastahili kuikatalia serikali na kuiambia (siyo kuiomba) ipange upya kama wanavyotaka.

  Hayo unayoyasema ya lobbying na influence ya mbunge ni kwa sababu kwamba sasa hivi inaonekana serikali ina nguvu kuliko Wabunge. Na kama kawaida mtu akisha kuzidi nguvu, njia rahisi ni kuwa rafiki yake. Utaona eti mbunge anajikomba kwa waziri ili asaidiwe jimboni. That is wrong and nonsensical!

  Una jaribu kusema Mbunge AHAKIKISHE, kwa vipi sasa ktk nchi kama hii ambayo wanaopigwa vita ni wale ambao wako vocal kuwasaidia wananchi na ni kwenye majimbo yao ndo eti tunaambiwa hawajaleta maendeleo. Mbunge alete maendeleo wakati kuna sabotage.

  Jaribu kukumbuka jinsi Serikali ilivyoanza kufanya sabotage ya majimbo yaliyokuwa yanashikiliwa na vyama vya upinzani huko Moshi na Mara. Sasa kidogo wamepunguza baada ya kuona haina manufaa kwao lakini bado inatumika kwenye majimbo na hata ya wenzao huko CCM.

  Kama kuna Mbunge ameshindwa kuwasilisha matatizo ya Wananchi wake Bungeni huyo kweli hafai, lakini kama amejieleza mara 1000 na serikali ikakaa kimya au ikakubali na baadaye haifanyi lolote eti watu wamchukie, hiyo ni failure ya Serikali ya CCM yote! Na kama wananchi wanamuona hafai hilo ni tatizo la uelewa mdogo wa wapiga kura wake.

  Mbunge ajenge shule, ajenge hospitali, ajenge barabara za rami, n.k.! Serikali ifanye nini sasa!

  Ndugu yangu kumbuka serikali iko ngazi zote kuanzia wilaya na huko ndo bajeti na mipango mingine huanzia. Kwa mfumo wa TZ Mbunge ni mjumbe wa Baraza la Madiwani. Baraza hilo hukaa pamoja na viongozi wa serikali na kutoa mapendekezo ya jimbo au Wilaya. Watendaji wa serikali hupanga na hayo yote hupelekwa juu mpaka ngazi ya Wizara ili yafike Bungeni na hapo tena Mbunge hukutana nayo.

  Najitahidi kueleza haya yote uone umuhimu na matatizo ya Mbunge ambayo ni ya kiutendaji na yale ambayo ni ya mfumo wa nchi. Ushauri wangu ni kwa Wilaya au majimbo kuhakikisha wanapata Mbunge mwenye Elimu na ufahamu ili aweze kuwasaidia madiwani huko halmashauri maana kuna gap (mara nyingi) kubwa sana kati ya Mkurugenzi akiwa na watendaji wake ukilinganisha na elimu ya Madiwani. Wakurugenzi wengi sasa hivi ni wenye degree za masters, Vipi madiwani?

  Ni mengi hatuwezi kuyamaliza hapa.
   
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Paragraph ya kwanza na ya pili ipo sahihi...ya tatu ni wewe kushindwa kuelewa! Unapoambiwa kampuni za sigara zinafanya lobbying unadhani ina maana gani? Lobbying ina exist in countries which are considered democratically developed, mfano Marekani, ambazo serikali haina nguvu zaidi ya bunge. Sasa wewe unaposema kuwa lobbying inaonyesha nguvu ya serikali nashindwa kuelewa. Lobbying is just one of tactics. Kwa nchi kama Tz ambapo mbunge anakuwa sabotage, inapidi tutafute mbinu mpya. Kwa mfano, mbunge kutumia muda mwingi kuelemisha wananchi wake kuhusu mapambano ya kuleta mahitaji yao. Sasa mbunge anapohama jimbo na kuwa na ofisi dar...kweli hiyo ni akili?
  Mimi sijasema mbunge ajenge shule,...nimesema mbunge ahakikishe kuwa analeta hizo shule. Kama serikali inampiga mgongo anaweza kutumia private sector. Kuna means nyingi tu...sema ni uvivu wa kufikiri na kushindwa kazi. Kwa mfano, serikali ikishindwa kupitisha bajeti...lazima ianguke! Kwa hiyo mbunge ambaye serikali inagoma kusikiliza hoja yake, ana 'uwezo' wa kuangusha serikali! hapa utaongelea idadi inayohitajika kuangusha/kupinga bajeti...na mimi nitajibu lobbying. Mbunge akijipanga na wenzake ambao serikali haitaki kuwasikiliza, basi huo ndo utakuwa mwisho wa hiyo serikali. Lakini there is a catch kwa Tz...KATIBA. Serikali inaundwa na Chama chenye wabunge wengi! Chama kina uwezo wa kumfutia mtu uanachama. Huwezi kuwa mbunge bila kuwa na Chama. Kwa hiyo, ukipingana na Chama, kina uwezo wa kukutoa bungeni! Unaona mzunguko huo? Kwangu mimi hili ndilo tatizo!!
   
Loading...