Upendo wa mama wazidi wote

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,028
Reaction score
168,647

Picha hii ilipigwa mwaka 2013 katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara, nchini Kenya na mpiga picha za wanyama (wildlife photographer) Alison Buttigieg, na ilishinda kuwa picha bora ya mwaka katika tuzo za habari huko Australia.
Swala huyu anayesulubiwa na Duma hawa, ni Mama wa watoto wawili. Akiwa na wanae kwenye maskani yao, walivamiwa na Duma waliokuwa na njaa. Watoto wake walikuwa wadogo na hawakua na nguvu za kuweza kukimbia na kujiokoa. Mama yao angaweza kuaamua kukimbia na kuwaacha wanae ambao wangeweza kuwa chakula cha Duma.
Lakini hakuwaacha alikimbia nao. Baada ya umbali kidogo akaona Duma wamemkaribia. Akaacha wanae waende na yeye akapunguza mwendo. Alitaka kuhakikisha wanae wanakuwa salama hata kama yeye atadhurika. Duma wakamfikia na kumparamia.
Katikati ya Duma wawili bado aliweza kusimama wima na kuwatazama wanae ambao walikuwa wakizidi kuyoyoma porini. Alikuwa akiwatazama kwa mara ya mwisho maana alijua hatawaona tena!!! Ilikuwa ishara ya kuwaaga.
Kwa macho yenye ujasiri aliwaaga wanae. Aliwakodolea macho hadi wakapotelea kabisa porini kabla ya kukubali Duma kumgeuza chakula. Alihakikisha kitu cha mwisho kuona kwenye macho yake ni taswira ya wanae. Ilikuwa ni ishara ya kuwaaga. Alijua hatawaona tena, lakini hakusikitika maana alijua kifo chake kilikua ukombozi kwa wanae.
Picha hii inatuonyesha taswira halisi ya Upendo wa Mama.
 
hayo maelezo yote aliyatoa uyo mpiga picha au kuna video na sisi tuione
 
Mkuu, hapo si kwamba kuna duma watatu? Lakini, si kila mama ana upendo kwa mtoto/watoto wake
 
Huyo ni Swala asokua na Akili.

Demu anaakili. Anatoa mimba, mara atupe mtoto ,mara amuite mwanawe Mbwa ,msengee ,pumbavuuu[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…