Upendo Peneza (CHADEMA) awalaumu Wabunge wanaohama vyama. Asema chaguzi za marudio ni kucheza pesa za wananchi!

Chadema sasa hivi ukipigiwa simu kama haipatikani tu wanavujisha unataka kuhama
Halii hii ya taharuki inawafanya chadema wasifikirie lollote kwa sasa zaidi ya kuwaza nani atakaefuata
 
Ndugu yangu inaonekana huwajui vzr ccm hakuna mtu anaehongwa hiyo Hela
hao wanauziwa maneno tu
 
Mwenyekiti wa CDM kupitia cheo cha KUB itisha kikao cha dharura cha Wabunge wa Chadema ilikuweka wazi msimamo wa Chama na wanachama. Wanaoondoka waondoka haraka !

Chama si mbunge wala Kiongozi kama Mbowe au Slaa au Zitto. Chama ni wanachama!

Na katibu mkuu aende mbali kwa kutoa waraka kwenda makatibu wa Wilaya ilikupata misimamo ya wanachama .

cc. Tumaini Makene
 
Huyu dada aliingizwa kwenye public na Kipanya Masoud kupitia Maisha Plus, upeo wake wa kuelewa mambo na kuchanganua kwa hakika inaonyesha wazi kuna akili kubwa (iliyomfunda) nyuma yake!
 
Na waliomsifia ana akili, watarudi kwenye kumponda tena! Ndivyo siasa za kitanzania. Ujinga na unafiki mtupu!

Kwa alivyozungza hata mia mwana ccm , namsifu anstahili nyadhifa aliyonayo. Ni Mtanzania mwenye msimamo. Ingependeza chama chake kimkuuze vizuri NA wasimpoteze
 
Ndo maana kuna wafuasi wanaitwa nyumbu.kabla hajaongea chochote walianza kumponda na kejeli kibao na wakafika hadi kuingiza ukanda ooh sio ajabu coz ni kanda ile Mara ooh viti maalumu mwache aende nk.Kaongea tofaut tayar matusi na vijembe vimepotea na sasa ni sifa kedekede.MWANASIASA MZURI HUWA NA AKIBA YA MANENO sio mropokaji.
 
Hizo ndo siasa zetu zinapoendeshwa kwa njama na unafiki: CHADEMA walimpokea Wema na kumzungusha hadi viwanja vya michezo ikiwa ni kuwakomoa CCM. Wakampokea Nyarandu na kumfanya shujaa bila kumbukumbu ya pesa za walipa kodi. Sasa imekuwa zamu yao kupoteza, limeuma! sasa tunaambiwa pesa za walipa kodi.

Lini vyama hivi vimekuwa na uchungu wa pesa? Tuliko mtaani ndo tulistahili kuwafokea na kusema upuuzi wenu unatutia hasara lakini bahati mbaya sisi tulioko nje tunawasaidia kuzomea na kushangilia vituko vyenu wanasiasa! Shame!
 

Uko sahihi! Uzabinazabina huu wa Mitandaoni ukiachwa hivyo ni shida
cc. Mnyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…