DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mkuu wa kitengo cha hamasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao makuu Upendo Peneza amejitosa kuomba ridhaa ya chama kuwania nafasi ya Ubunge jimbo la Geita mjini Mkoani Geita.
Hii ni mara ya pili kwa Peneza kuomba nafasi hiyo ambapo mwaka 2020 aligombea jimbo hilo kupitia Chadema lakini hakufanikiwa, sasa anarudi tena kwenye kinyang’anyiro hicho akiwa ndani ya CCM.
Alijiunga rasmi na CCM Januari 22, 2025, baada ya kukihama Chadema ambako alikuwa Mweka Hazina wa Kanda ya Ziwa Victoria.
Ikiwa atapitishwa na chama, atapimana nguvu na aliyekuwa mbunge wa sasa, Costantine Kanyasu, pamoja na wengine wanaoendelea kuchukua fomu ndani ya CCM.