Upendo Nkone: Hata mimi na mume wangu tunagombana

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Watu wengi huwa wanapata picha kuwa watu wa dini, wachungaji, waimbaji wa nyimbo za injili kuwa huenda wao maisha yao ya ndoa huwa yanakuwa na amani na furaha tupu lakini mwimbaji Upendo Nkone anasema hilo jambo si kweli.

Msanii huyo wa siku nyingi katika anga la muziki wa injili Tanzania amesema yeye na mume wake ambaye ni mchungaji kuna wakati wanakokorofishana, kununiana na hata kugomabana.

Upendo Nkone aliyasema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachofanyika kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni, ambapo amesema hadi sasa ndoa yake ina miaka sita.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili anakiri kuwa kuna wakati inafikia kutozungumza na mumewe hata kwa mwezi mzima licha ya kuishi katika nyumba moja ambapo sababu mojawapo huwa ni kutokana na tabia yake ya kutopenda kupika chakula, jambo ambalo mumewe huwa linamkwaza sana.

"Tunagombanaga sometime tunalianzisha, tunafunga milango, tumeshanuniana karibu mwezi, kwa mfano unakuta kuna siku sijapika, huo ndiyo ugomvi mkubwa na mume wangu, akipika dada halafu kama akikuta chakula akijakaa sawa, hapo sasa ndiyo utamjua Mbena ni nani, hatujawahi kupigana makofi lakini kuna wakati aliwahi kunikunja.... kama unavyojua wanaume hampendi kudharauliwa" amesema Upendo

Ameendelea kusimulia "kuna wakati nikiona ameshakasirika nakuwa karibu na mlango.... halafu akishuka najisemesha semesha...mimi mume wangu huwa namuamkia, shikamoo baba, maana amenizidi umri"

Amesema aliamua kuolewa na mtu mzima kwa kuwa alimuomba Mungu ampe mtu mzima kuliko yeye "ili nijifeel like a baby" badala ya kuwa na vijana wenzake.
 
Safi sana nkone ameongea ukweli kabisa bila kupepesa mdomo
 
Weka picha
JF expert member.... Basi sawa... Halafu wakija wengine kuandika yasiyopendeza utasiki... KAKOJOE UKALALE, SHULE ZIMEFUNGULIWA ..... napata shida sana nitumie maneno gani yanayofanana na hayo hapo juu kumweleze JF EXPERT MEMBER ili ujumbe ufike kama ulivyokusudiwa....
 
Kugombana ni sehemu ya mapenzi na maisha ya binadamu so kikubwa ni kusameheana na kutambua wajibu wa kila mmoja
 
Back
Top Bottom