Super Sub Steve
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 17,719
- 11,333
Watanzania kwa kulalamika!Toka zoezi la kupata chanjo lizinduliwe rasmi kuliwekwa vipaumbele kwa makundi matatu.
Kwanini wasingesema Kila mtu ambaye yupo tayari kupata chanjo apate?
- Waliofika miaka 50 na zaidi
- Wahudumu wa afya
- Wenye magonjwa ya Mara kwa mara
Halafu Kuna watu hawajafika 50, si wahudumu wa afya na huenda hawana magonjwa ya Mara kwa mara wanapata chanjo, kwa mfano
Shaka (Wa CCM) hajafikisha 50 na Wala sio mhudumu wa afya lakini kachanjwa.
Jokate Mwegelo, na wengine.
Sasa sisi wengine tukienda kuchoma mbona tunakataliwa. Tuliopo tayari wangeturuhusu tuchome kwa vile Ni hiari na imani chanjo zilizopo zingetufaa.
My Take:
Kitendo Cha kutuzuia wengine kuchoma chanjo napata wasiwasi huenda akina Gwajima akina Polepole wanatumika na Serikali ili kuficha aibu ya serikali kuishiwa chanjo mapema.
Nipo Dar nimeenda leo kituo Cha afya Magomeni nimekataliwa pia kuna kituo kingine niliongea na mmoja wa wahudumu wa pale kabla ya kwenda akaniambia ukija kwetu hutachoma kwa vile hujafikisha 50 ndo nikaamua kubook Magomeni.Kufika Magomeni napewa jibu lilelile kuwa kwa Sasa Sina sifa ya kupata chanjoWewe uko wapi mbona nasikia watu wanachoma kwa uhuru tu bila changamoto yoyote.
Wanaweka hamasa kwani watu hawataki kuchoma? Kama hawataki kuchoma si waseme ruksa Kila mtu kuchomaWatanzania kwa kulalamika!
Umeambiwa na viongozi wanatakiwa kuchanja ili kuweka hamasa
Wenye umri mkubwa ndio wanachoma kwa Sasa.Inasemekana watu wenye umri mkubwa hawaonyeshi sana side effects za chanjo kama vijana.
Viongozi wanatumia nguvu kubwa kuhamasisha watu wasiohamasika na wakati huohuo wanatuzuia watu tuliokubali pasipo kuhamasishwa,Kama watu hawataki waachane nao waturuhusu tulio tayari tuchomeWatanzania kwa kulalamika!
Umeambiwa na viongozi wanatakiwa kuchanja ili kuweka hamasa
Yeah ila nazungumzia huko kwa wenzetu waliyokwisha tangulia kuchanjwa.Wenye umri mkubwa ndio wanachoma kwa Sasa.
Njoo BagamoyoNipo Dar nimeenda leo kituo Cha afya Magomeni nimekataliwa pia kuna kituo kingine niliongea na mmoja wa wahudumu wa pale kabla ya kwenda akaniambia ukija kwetu hutachoma kwa vile hujafikisha 50 ndo nikaamua kubook Magomeni.Kufika Magomeni napewa jibu lilelile kuwa kwa Sasa Sina sifa ya kupata chanjo
Bagamoyo mjini au kituo gani Hakuna longolongo?Njoo Bagamoyo
Subiri kaka kuna zigo linakuja wewe haupo kwenye hatari ya kuambukizwa,acha 50+ wamalizike na makundi maalumViongozi wanatumia nguvu kubwa kuhamasisha watu wasiohamasika na wakati huohuo wanatuzuia watu tuliokubali pasipo kuhamasishwa,Kama watu hawataki waachane nao waturuhusu tulio tayari tuchome
Chelewachelewa utamkuta mwana si wakoSubiri muda utafika utachanja usiwe na haraka na maisha
50+ wenyewe baadhi yao wanasikiliza maneno ya GwajimaSubiri kaka kuna zigo linakuja wewe haupo kwenye hatari ya kuambukizwa,acha 50+ wamalizike na makundi maalum
Hapa mjini ni akili tuu. Tumia akili yako hapoNipo Dar nimeenda leo kituo Cha afya Magomeni nimekataliwa pia kuna kituo kingine niliongea na mmoja wa wahudumu wa pale kabla ya kwenda akaniambia ukija kwetu hutachoma kwa vile hujafikisha 50 ndo nikaamua kubook Magomeni.Kufika Magomeni napewa jibu lilelile kuwa kwa Sasa Sina sifa ya kupata chanjo
Tayari dirisha kwa wote limefunguliwa50+ wenyewe baadhi yao wanasikiliza maneno ya Gwajima