Upelelezi wawakwamisha kina Kitilya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Upelelezi wa kesi inayomkabili Harry Kitilya na wenzake wawili, Shose Sinare na Sioi Solomon katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Kishenyi Mutalemwa alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 20, kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.

Katika kesi hiyo, Kitilya na washtakiwa wenzake wanakabiliwa na mashtaka manane, likiwamo la utakatishaji wa Dola 6 milioni za Marekani.

Chanzo:
 
Kitilya alishasahau hata kutumia choo cha kukalia. Papuch ndio anaisikia kwa bomba.
Juzi juzi tu alikua akinyanyua kidole TRA inatikisika.
Leo hii anashinda na kulala na common criminals. Hujafa hujaumbika
 
Whats your point buddy!!ndo uanaume huo
 
Hizo rangirangi kwenye sentensi zako unafanya kazi coral paints au?
 
Back
Top Bottom