Kesi zingine ni kukomoana tu, mlalamikaji yuko dar, wahasibu na wakaguzi wa mahesabu wako dar, kiwanda kiko dar na wapelelzi pia wako dar. Sioni sababu ni kwa nini upelelzi uchukue miezi miwili au mitatu.
Mahakimu wetu ni wagumu sana kutumia busara za kawaida kubaini kuwa hapa ni kukomoana, hasa ukizingatia kuwa sheria ya sasa inataka mtu adeposit nusu ya hela iliyoibiwa katika kesi hii ni shs 39millioni. Sheria ipo lakini kutokana na kuwa mahakimu wanashindwa kubaini kesi za uongo na ukweli wanakuwa wazito kutoa dhamana na au kufuta kesi.
Mwisho, vifungu vya dhamana inabidi viangaliwe na kurekebishwa vinafanya administration of justice kuwa mzigo mkubwa sana kwa serikali bila sababu yoyote.Matusi ndani bila dhamana, bangi weka ndani, wadada poa weka ndani, wapiga debe weka ndani. Kwa kila mtu mmoja anayekaa rumande mlipa kodi anagharamia dearly, so to speak.