Updates: Ufungaji bar saa 6 na muziki wa sauti kubwa Dar es Salaam

mpenda pombe

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
1,408
704
Hapo ulipo agizo la Rc Mh Makonda la kufunga bar saa 6 usiku na kutopiga muziki kwa makelele maeneo ya makazi limetekelezwa?

Hapa nilipo makumbusho, Royal bar, band ya taarabu inapiga kama kawa na kwa sauti ya juu..

Utekelezaji wa hili agizo ni mgumu Sana.

Hapo ulipo bar na muziki unapigwa?

Tuendelee na updates kwa wakazi wa dar..
 
Mud house in Tanzania, a Hut by KonstantinIk _ WikiHomes(1).jpg
 
Sasa lengo la kutafuta pesa kutwa nzima ni nini?
Sasa utafute pesa kutwa nzima ndo ukalewe hadi majogoo?? Kufunga bar saa 6 ndo mwake, hata majuu ni hivyo hivyo, ukitaka kukesha kuna sehemu zake kwa ma "night clubs" hadi majogoo lakini sio bar za kawaida.. Hio sheria ifuatwe tusitengeneze taifa la walevi.
 
Hays ndo athari za soko huria tulilea tatizo Na leo kutolewa agizo Watu waliona ni kama mastaajabu fulani.Sheria zilikuwepo na hazikuwahi kufutwa wala kubatilishwa na Bunge katika nchi hii.Ndo hivyo tena ni lazima zihiushwe na zifanye kazi wengi wetu hatujui wala hatuna uelewa wa kuwa sheria hizo zipo
 
Kamanda Siro alitoa tamko kwa mbwembwe... Siamini kama litatekelezeka.
 
ngoja tusubir tuone kama mh mkuuu wetu atakuja na gia nyingine
 
Back
Top Bottom