Yale mashindano ya Ligi ya jimbo cup maarufu kama Kagasheki Cup yanayodhaminiwa na Mbunge wa Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki yameanza kutimua vumbi leo katika uwanja wa kaitaba mjini Bukoba.
Ligi hii ina shamra shamra kubwa katika mji huo kuliko hata ligi kuu ya Vodacom.
Uzinduzi wa ligi hiyo umefanywa na Kagasheki mwenyewe. Ambapo amesema msindi wa kwanza atapata sh milioni 5,mshindi wa pili milioni 3 na wa tatu milioni 1.5 aidha kila timu itapata sh 500,000 za usafiri kwa timu zote 14 zinazounda jimbo hilo.
Picha za uzinduzi na taarifa nyingine fuatilia thread hii itakayokuwa na update juu ya ligi hii hadi itakapomalizika.
....................Keep watching...............