Updates: Hukumu kesi ya EPA leo

bibikuku

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2011
Posts
832
Reaction score
496
Wana JF

Leo Mahakama inatarajia kutoa hukumu nyingine kesi ya Rajab Maranda na Farijala Husein kuhusu wizi wa shilingi karibu bilioni 2 za EPA. Wenye uwezo wa kupata updates twaomba mtupatie hapa
 
Hapo hukumu inajulikana kabisa.

Mahakama zao,majaji wao,
unategemea nini hapo?
 
dagaa ndo wengi-maneno ya hoseah haya si yangu

Ni lazima usafishe mtandao kwa kuanza na dagaa. Hata sinema huwa tunaona kwanza wanamalizwa maadui halafu ndio anasakwa kubwa la maadui. Uliona sinema ipi "gang leader" akamalizwa mwanzo, si sinema itakwisha kabla haijaanza.
 
Kesi gani hiyo mshitakiwa namba moja, 50,000,000,000 hayumo.
 
wamejaa tele. lakini dagaa ndio wanaomalizikakwanza ndipo nyangumi wafuate

Mkuu ulimsikia yule mkurugenzi jana anadai nyangumi baharini sio wengi ndio maana wanahangaika na hivi vidagaa !
 
Ni lazima usafishe mtandao kwa kuanza na dagaa. Hata sinema huwa tunaona kwanza wanamalizwa maadui halafu ndio anasakwa kubwa la maadui. Uliona sinema ipi "gang leader" akamalizwa mwanzo, si sinema itakwisha kabla haijaanza.

acha ngonjera wewe,kwenye movie huwa wanafanya vile ili lengo litimie wewe unataka movie ikianza tu kubwa la maadui afe,halafu na movie iishe au? Hapa inapaswa mkubwa ndio ashughulikiwe kwanza ili wale wadogo waache mara moja kwani wakiona mkubwa kashughulikiwa wataogopa..Yaani litokee dubwana kubwa limmeze tembo we unafikiri swala atalisogelea?
 
Aliyekulamba billion mbili unamwita kidagaa? kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Aliyekulamba billion mbili unamwita kidagaa? kwi kwi kwi teh teh teh!

zomba punguza mapenzi na magamba sio kila kitu unaunga mkono, hao si lolote si chochote tunataka wale walio eng
ineer hii kitu na wasiishie hapo wote bila kuwaangalia usoni waliohusika na Rada,Kiwira,Richmond e.t.c
 
Pesa iliyoibwa EPA ni zaidi bil 40 tunahangaika na 2bil. wako wapi walioiba bil 20?
Asalamaleku walah
 
Aliyekulamba billion mbili unamwita kidagaa? kwi kwi kwi teh teh teh!
wakati kuna watu wanauwawa kwa kuiba simu za mchina zenye samani ya 50000....hivi hizo bilioni zaidi ya 2 zinge pelekwa hospitalini au mashuleni zinge saidia kiasi gani? tuache unafiki
 
Pesa iliyoibwa EPA ni zaidi bil 40 tunahangaika na 2bil. wako wapi walioiba bil 20? Asalamaleku walah
Sasa ulitaka mkuu wa nchi ashitakiwe hii itakuw kazi ya kwanza ya chadema wakiingia madarakani lakini kwa wana-CCM hawawezi....
 
wakati kuna watu wanauwawa kwa kuiba simu za mchina zenye samani ya 50000....hivi hizo bilioni zaidi ya 2 zinge pelekwa hospitalini au mashuleni zinge saidia kiasi gani? tuache unafiki

Tatizo lako unashindwa kuelewa kuwa mabunge yetu ndio yanayoweka hizi sheria na si mimi wala wewe. Labda mwenzangu ni mbunge.

Sheria zetu na nyingine nyingi duniani, zinazotungwa na watu (wabunge) zimejaa kulindana, hapo bungeni wale unaowaona usifikiri kuwa wako pale kwa maslahi yako wewe zaidi, wako pale kwa maslahi yao na kujilinda wao kwa wao, si wa upinzani wala wa chama tawala.

Hivi, umeshajiuliza ni kwanini wanaowaua waiba simu hawachukuliwi hatua? nini kinachowalinda? utakuta ni wewe mmoja wapo unaowalinda hao wauaji wa mitaani, akitokea mwizi akauliwa na wewe upo kwenye eneo, unajuwa kabisa ni fulani na fulani ndio waliomuuwa, lakini unakaa kimya huendi kuwashitaki wala kupeleka ushahidi. Halafu leo uozo huohuo unautolea mfano?

Wizi upo, haukuanza leo Tanzania hii, cha kutia moyo ni kuwa angalau kwa sasa tunaona hao wizi wa "EPA" wakifikishwa mahakamani. Kumbuka kuwa hii EPA ni madudu ya awamu iliyopita na walikuwepo watunga sheria pia, walikuwa wapi? mpaka aje Kikwete ndiyo ayaibuwe na kuisuka PCCB upya?, hivi kabla ya PCCB kulikuwa hakuna hivi vyombo vya kuzuwia rushwa? vilikuwa wapi? vilifanya nini? vilimfikisha nani mahakamani? majibu ni rahisi kabisa. Hakuna.

Leo hii yule anaechapa kazi na kuyaibuwa yote haya na kuchukuwa hatua stahiki za kubadilisha sheria za kulindana na kufumuwa mitandao ya huu wizi na mwingine ndiye anaonekana hafai. Ajabu sana.

Kumbuka kuwa sheria zimebadilishwa sana kipindi cha Kikwete zimeziba mianya mingi iliyopo awali na pia ukumbuke kuwa hivyo ni vita endelevu, ni uozo ulioota mizizi na kuuvunja na kuuondoa huo uozo kwa siku moja ni ndoto. Lakini matumaini yapo na ni mema sana na tumeona nia safi ya Kikwete katika awamu yake ya uongozi.
 
Ni lazima usafishe mtandao kwa kuanza na dagaa. Hata sinema huwa tunaona kwanza wanamalizwa maadui halafu ndio anasakwa kubwa la maadui. Uliona sinema ipi "gang leader" akamalizwa mwanzo, si sinema itakwisha kabla haijaanza.

Kweli kabisa wakome kuvamia mambo wasioyaweza wala kuyajua.
 
Miaka inaenda wale mapapa wanadunda tu mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…