Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
UPDATES KUHUSU KESI ZA YERICKO NYERERE*
Yericko Nyerere alikamatwa na Polisi siku ya J'5 tarehe 31/05/2017 usiku na kuwekwa Mahabusu Central Police DSM. Hakupelekwa Mahakamani hadi Ijumaa tarehe 02/06/2017 ambapo alifunguliwa shitaka lile lile la Kesi iliyofutwa. Baadaye alipata dhamana lakini alibaki mikononi mwa Polisi kwa madai kuwa alihitajika kwenda kutoa maelezo Central Police kuhusu shauri lingine.
Waliendelea kumshikilia na hata tulipohitaji kumtoa kwa dhamana, wali...dai haiwezekani kwa kuwa faili lake lilikuwa kwa DPP na kwamba angefikishwa Mahakamani J'3. Ilipofika J'3 tarehe 05/06/2017 wengine tukiwa Msibani Moshi, wadhamini wakiongozwa na Katibu wa Jimbo la Kigamboni kamanda Simon Magese walifika Mahakamani lakini hakuletwa.
J'4 alipoletwa Mahakamani kwa ajili ya Kesi ya awali kutajwa kwa mara ya kwanza, shitaka jipya halikusomwa. Mawakili wetu nguli Tundu Lissu, Hekima Mwasipu na Jeremiah Mtobesya walicharuka na hivyo kupelekea Mahakama kutoa amri ya Mtuhumiwa kuletwa Mahakamani kesho yake, yaani J'5 (jana). Jana hakuletwa kwa madai kuwa hawakuwa na taarifa juu ya amri hiyo ya Mahakama.
*YERICKO MAHAKAMANI LEO TAREHE 08/06/2017*
Leo tena tuligawanyika, wengine tukawa Central na wangine wakawa Kisutu. Ameletwa _Mahakamani mchana huu._
*_Wadhamini na mawakili wasomi (Jeremiah Mtobesya na Hekima Mwasipu) wapo_* , tunaongoja shauri kupangiwa Hakimu tuingie.
Solidarity forever!
---------------------------------
*Mbusule C. Shillu*
_Afisa Oganizesheni na Uchaguzi Kanda ya Pwani_