Upatikanaji maji salama bado ni duni sana nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upatikanaji maji salama bado ni duni sana nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 24, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Leo ni siku ya maji ya duniani. Hapa nchini maadhimisho hayo yalifanyika kwa wiki nzima kuanzia Machi 16, mwaka huu na kuadhimishwa kitaifa mkoani Iringa.
  Kumekuwa na harakati mbalimbali zinazofuatana na maadhimisho haya ambayo yamekuwa ni ada ya kila mwaka.
  Kikubwa ni kukutanisha wadau wa maji wa aina mbalimbali na kujitafakari wapi tulikotoka, tulipo na tunakokwenda kama taifa kufikia malengo ya upatikanaji wa rasilimali maji nchini.

  Sera ya taifa ya maji ya mwaka 2002 inaainisha malengo makuu kuwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wake ni wa uhakika ili kuinua hali ya maisha ya watu wetu; kuongeza upatikanaji wa rasilimali hiyo kwa ubora unaotakiwa ili kuchochea uzalishaji katika sekta nyingine kama za viwanda, nishati na migodi; kuongeza na kuwa na uhakika wa maji ya matumizi ya binadamu pamoja na umwagiliaji na mifugo, kwa pamoja eneo hili litahakikishia taifa uhakika wa chakula.

  Lakini pia juhudi za kuongeza upatikanaji wa maji bora na karibu zaidi na maeneo ya makazi itasaidia kupunguza adha na ugumu wa maisha kwa wanawake na watoto ambao wanatembea muda mrefu na kwa saa nyingi kusaka maji kwa ajili ya matumizi ya familia, upatikanaji wa uhakika wa maji utasaidia pia hifadhi ya mazingira kama vile upandaji wa miti na kuhifadhi vyanzo vya maji hivyo kuhifadhi mazingira kwa maana pana.

  Takwimu za upatikanaji wa maji nchini zinaeleza mafanikio makubwa, kwamba taifa limefikia juu ya asilimia 80 ya wakazi wa mijini kupata maji salama, wakati vijijini viwango ni vya chini kidogo
  Takwimu za serikali za upatikanaji wa maji kwa mwaka 2010 zinaonyesha mafanikio makubwa kwa kipindi cha miaka mitano kati ya 2005 hadi 2010; watu wa vijijini waliofikiwa na maji salama ni asilimia 58.3 huku viwango vya mijini vikielezwa kuwa ni asilimia 80.3. Malengo hadi kufikia mwaka 2015 ni makubwa zaidi kuliko hali ilivyokuwa mwaka juzi.
  Pamoja na kuwako kwa programu ya maendeleo ya sekta ya maji, bila kusahau hatua zinazoelezwa kuwa zimepigwa; hali halisia ya upatikanaji wa maji salama kwa mijini kama ilivyo vijijini ni mbaya.
  Huduma ya maji katika maeneo mengi ambako awali ilikuwa nzuri imezidi kuporomoka mwaka hadi mwaka, wakazi wa mijini waliokuwa wamefikiwa na mtandao wa maji ya mabomba, sasa wanaishia kununua maji kwa madumu ambayo hata hivyo usalama wake ni wa kutiwa shaka mno.

  Ni ukweli usiokuwa na chembe ya shaka kuwa mwaka baada ya mwaka hali ya upatikanaji wa maji mijini sawa na vijijini inazidi kuwa mbaya; harakati za wananchi ama mmoja mmoja au kupitia vikundi nazo hazijazaa matunda makubwa sana katika kujitafutia huduma ya kuaminika ya maji kwa sababu kimsingi utengenezaji wa maiundombinu ya maji huhitaji gharama kubwa, hivyo mkono wa serikali ni muhimu.

  Ukipita katika mitaa ya miji mingi ya nchi hii, ikiwamo ile mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na mingineyo, shughuli ya kuhemea maji imekuwa ni changamoto kwa familia mbalimbali, wakazi wengi wanaishi kwa kubaingaiza maji; hakuna uhakika wa maji, bado watu wetu wanasumbuliwa na magonjwa yanatokana na matumizi ya maji ambayo si salama.
  Kimsingi changamoto ya kupatikana kwa maji salama kwa watu wengi zaidi na kwa uhakika inazidi kuwa kubwa kadri tunavyosonga mbele; haya yanatokea wakati vyanzo vya maji vikiwa dhahiri kabisa. Pamoja na kelele za kitakwimu zinazotolewa na watawala, bado hali halisi ya upatikanaji wa maji si ya uhakika na kuridhisha kama inavyoelezwa.

  Ni kwa hali hii tunasema kama taifa wakati tukiungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya maji duniani, tunapaswa kuwa wakweli, kutambua changamoto hii, serikali ikubali kuelekeza rasilimali nyingi zaidi katika kutatua changamoto hii.
  Ni hakika wakazi wengi wa mijini wanazidi kuondoka kwenye kundi la watu wenye uhakika wa maji kadri siku zinavyokwenda, kwa wale wa vijijini hali ni mbaya zaidi. Tunataka Mapinduzi ya kweli katika sekta ya maji na si utoaji wa takwimu zisizoeleza hali halisi.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...