Adui mkubwa wa Ulcers ni MAWAZO, ukiwa mtu mwenye mawazo na masononeko utaumwa weye hadi ujikatie tamaa,
Badili Mfumo wako wa chakula kwa kuepuka kula vyakula vinavyochochea Acid tumboni,
Mawazo na Hasira vinachochea sana uzalishaji wa Acid,
Umetumia dawa nyingi sawa je hizo dawa umetumia kwa Muda gani? Maana wengi hutaka kutumia Dawa wiki mbili anataka awe amepona bila kujua ugonjwa aliokua nao niwa siku nyingi kwa maana hiyo na matibabu yake lazima yachukue muda mrefu,
Anza Dozi ya BAMIA, Bamia ni kiboko kwa Peptic Ulcers, ni simple dozi isiyo na gharama wala kupoteza Muda, unachukua Bamia zako unazikata kata vipande vidogo unachemsha kiasi unaweza kuweka chumvi kidogo kuleta ladha kisha unakunywa kikombe kimoja asubuhi mchana na jioni au asubuhi na jioni kila siku kwa miezi mitatu mfululizo baada ya hapo unaenda kupima, daktari lazima aone acid imepungua so unaweza kuendelea kwa miezi mitatu mingine,
NB: Ukianza kutumia Bamia utapata matokeo ya haraka usiache dozi kwa kujihisi umepona endelea kwa miezi hiyo mitatu.