Uozo Wizara ya Afya

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,091
1,177
Ukweli ni kwamba tatizo lililopelekea mgogoro na mgomo wa madaktari ni uongozi mbovu wa Wizara ya afya.

MAT (Chama cha Madaktari) walilenga kuelezea hali ilivyo ikiwamo kucheleweshwa posho za madaktari, Wizara kukata sehemu kubwa ya mafungu (kasma) ya Hospitali, ubinafsi wa Watendaji Wizarani, na matatizo yaliyopo kwa ujumla n.k.

MAT walifanya kila jitihada kuomba kuonana na Uongozi wa Wizara ya Afya ili kuepusha mgomo kwa kupatia ufumbuzi matatizo yaliyopo, lakini si Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu wala Mganga Mkuu aliyekuwa tayari kuwasiliza. MAT walikumbana na kejeli, na dhihaka kutoka kwa Viongozi hao wa Wizara yao.

MAT waliposhindwa madaktari wakaamua kulichukua suala hilo na kuomba kuonana na Uongozi wa Wizara. Hata hivyo hila na fitina ziliendelea na hivyo nao pia hawakufanikiwa.
Madaktari wakaomba kuonana na PM Pinda. Waziri wa afya alipopata habari hiyo akawahi kwa PM na kufanya fitina. Akampotosha PM kuhusu ukweli wa mgogoro ulivyo.
Kutokana na kupotoshwa na Waziri wa Afya, PM akatumia hatua zisizofaa kutatua mgogoro kwa kutoa vitisho kwa madaktari. Pia aliagiza kupelekwa madaktari wa JWTZ kusaidia MNH hali iliyosababisha madaktari bingwa nao kuingia kwenye mgomo.
Maafa yaliyotokea sio madogo, tumewapoteza ndugu zetu wengi kutokana na hujuma, hila, fitina na Uongozi mbovu wa Wizara ya Afya.
Hata hivyo PM Pinda alipata ukweli ulivyo baadaye, baada ya madhara makubwa kutokea. Alipewa ukweli kuhusu hujuma, hila, fitina na upotoshwaji uliofanywa na Waziri wa Afya Mponda.

Alipoongea na madaktari jana (Feb 09, 2012) PM alitumia lugha tofauti na awali. Na pia alionyesha wazi kujua tatizo lilipo na jinsi alivyopotoshwa. Aidha alijulisha kuwa amepata taarifa za uozo uliopo Wizara ya Afya.

PM alichukua hatua ambazo tumejulishwa. Lakini ukweli ni kwamba, hata kama Waziri Mkuu angeamua kutoongeza posho na badala yake kuwawajibisha viongozi hao wabovu wa wizara akiwemo Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Mganga Mkuu, ni wazi kuwa madaktari wangefurahi, wangeridhika na wangerejea kazini kwa moyo mmoja.

Lakini pia hata kama PM angeamua kuwaongezea posho kwa mara 10 ya kiwango walichohitaji madaktari, na kuwaacha hao viongozi wabovu wizarani, ni wazi kuwa madaktari wangeendelea na mgomo.
Uongozi wa wizara ya afya umesababisha maafa, umelisababishia taifa la Tanzania aibu na fedheha kubwa, na pia umeigharimu serikali na walipa kodi gharama ambazo waliwajibika kuziepusha kwa makuwa wasikivu.
Tuendelee kuishinikiza serikali kuisafisha Wizara muhimu ya afya. Lakini pia serikali isipende kusubiri mpaka maafa yatokee ndipo ichukue hatua.
Wenye nafasi walisimamie hili.
 
SAWA ! LAKINI BAHATI MBAYA TULIKUWA NAYO HAKUNA KITAKACHOFANYIKA! JAIRO YU WAPI NA HATA NYOMI AH SIJUI NYONI MTASIWA WATAPITIA HUKO HUKO NA ISSUE ITA DISSOLVE KAMA KAWAIDA. HII NCHI INAENDESHWA KIKAMATI KAMATI TU ! LABDA NIULIZE TU TANGU AWAMU HII INGIE MADARAKANI MIAKA SABA ILIYOPITA NI MAMBO MANGAPI YALIOIBULIWA TENA YAKAWA YANA CONCRETE EVIDENCE LAKINI HAYAJATOA MREJESHO ZAIDI YA RIPORT ZA KAMATI TU! HATA HILI MWISHO WA SIKU UTASIKIA LIMEKWISHA KWA NJIA AMBAZO HATA NYIE WANANCHI MTAZIFURAHIA TU. RICHMOND IMEISHAJE WAKINA SITA NA MWAKYEMBE SIO WALIKUWA MASHUJAA PALE BUNGENI! LEO MBONA MNAWAITA WANAFIKI NA MAJINA MENGINE MABAYA TU! yetu macho na masikio tunasubiri
 
Kama kuna mtu anadhani JF tumemalizana na wizara hii kuhusiana na suala la madaktari wetu na uboreshaji wa mazingira yao ya kazi ili nasi tupate uhakika wa tiba bora, atakua amejidanganya.

Hakuna mbinu za zima moto hapa; tunasubiri sana kuona ahadi za Waziri Mkuu kwa madaktari hiyo 'baada ya mwezi mmoja' na kubwa zaidi ni kwamba tunasubiri kusukwa upya kwa sera ya sekta hii kuendana na mwenendo mzima wa soko huria na serikali kubakia kuwa mshauri na refarii tu.

Katika hili 'Mtoto wa Mkulima', hatujabanduka hapa bado.
 
Hayo yaliyoandikwa ndiyo ya kweli. Tatizo ilikuwa ni uongozi wa wizara na madaktari waliuwa wanataka waondolewe ili roho zao ziwe radhi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom