Uongozi wa serikali mkoa wa Morogoro ni jipu kubwa;vMagufuli safisha mkoa huu

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,600
3,651
Mkoa wa MOROGORO ni kati ya mikoa iliyo nyuma sana kimaendeleo na kiuwajibikaji. Njoo manispaa ya Morogoro ujionee jinsi manispaa ilivyochafu. KIPINDUPINDU kimeng'ang'ania manispaa ya MOROGORO kutokana na uchafu uliokithiri.
Pita maeneo ya soko kuu la mjini, utakutana na TOPE la haja wakati wa mvua au VUMBI la hatari wakati mvua imekatika.
Barabara za lami ndani ya manispaa zimejaa mashimo makubwa kiasi cha kuhatarisha usalama wa vyombo vya usafiri.
Viongozi waliopo hapa sijui wamerogwa? yaani wapo wapo tu.
Rais MAGUFULI nakuomba safisha uongozi kuanzia ofisi ya RAS, RC na Mkurugenzi wa Manispaa ili kunusuru hali mbaya iliyopo Morogoro.
 
Kuna chemba ya maji taka maeneo ya Faraja Trust Fund inatiririsha maji taka na yanatuama mferejini kwa muda mrefu sasa hakuna anayeshughulika. Na ni mita chache tu kutoka ofisi za manispaa, yani Morogoro imeoza kwa kweli
 
kampeni iliyopo mji kasoro bahari ni kusitishwa kwa huduma za chips na mama ntilie mji mzima, uchafu mji huu ni kero. mji mchafu na utupaji taka ovyo, yale maji machafu toka boma road mpaka stend yapo hai na hakuna action yoyote.......
 
Sio morogoro pekee
Kifupi mikoa yote I nahitaji mapinduz makubwa ya kiutendaji
 
Mi nmpitaji mzuri wa hii njia ya station road, hasa hapa karibu na savoy hotel bana pana wakati chemba za waarabu zinatiririsha maji taka hatari na pana madimbwi ya maji na mvua hii usoni kabisa mwa ofisi za station za reli hapa sijui hua hawaoni? M/kit wa mtaa ule nae sijui vp yaan!!
 
Morogoro mkoa unalaana ule.....hakuna mabadiliko yoyote miaka karbu 10 nimeujua upo vile vile zaidi ni gest tu zimeongezeka
 
Maeneo ya wazi kibao watu wamevamia.
Niungane nawe Lazalaza, haliya Morogoro nimbaya! Viwanja vya wazi ki!a mahali vimsuzwa. Mipango miji ipo karibu zaidi na iljyowauzia maeneo ya wazi. Shida kubwa.

UONGOZI WA MANISPAA NI KAMA HAUPO. LUKUVI TUNAO BA UJE UTUSAIDIE
 
Mbunge wenu tajiri hana msaada?
Acheni kuchagua viwavi ili mpate maendeleo.
 
Sio morogoro pekee
Kifupi mikoa yote I nahitaji mapinduz makubwa ya kiutendaji
Mfano Wilaya ya Kinondoni imejaa uchafu, mkuu wa wilaya siku nzima hafanyi kazi ni kushinda kwenye Mitandao kuchafua watu kumwandama kubebea na voja vingi.
 
Morogoro mkoa unalaana ule.....hakuna mabadiliko yoyote miaka karbu 10 nimeujua upo vile vile zaidi ni gest tu zimeongezeka
Wanapenda kuzaa sana, mvua ikinyesha tu guest zote zinajaa licha ya kuwa nyingi kila kona, hakuna mipango miji Ujenzi mwingi upo hovyo hovyo kuna Majipu kibao Ofisi ya Ardhi.
 
Back
Top Bottom