Kwanza kabisa kwa nafasi ya upekee kabisa ninaomba niwapongeze makamanda tuliowapa ridhaa ya kukiongoza chama huku jimboni Ukonga. Kimsingi CDM kimekuwa chama chenye nguvu katika maeneo yetu lakini tulikosea sana katika kumsimamisha mgombea wa Ubunge Jimbo la Ukonga mwaka 2010, Mzee Binagi ambaye naweza kusema hakupiga kampeni kabisa na kura alizozipata ni kwa sababu wananchi walikuwa wanahitaji mabadiliko yalioletwa na CDM karibu nchi nzima. Mbunge wetu aliyepo hakuna anachokifanya zaidi ya kusinzia Bungeni wananchi wanapata tabu za barabara husuani wale wanaokaa Mombasa kuelekea Moshi Bar, Kivule Mpaka Msongora, watu wa Mongora Ndege hawana daraja la uhakika lakuvukia Mto msimbazi wakati wa Mvua ni baraa tupu. Wahanga wa mabomu wa Gongolamboto mpaka leo hawajafidiwa mpaka leo wanabaki kuhangaika. Migogoro ya Ardhi katika maeneo ya Chanika na Kivule kuelekea Msongora, kutokuwa na soko la uhakika katika eneo letu la Ukonga.
Pamoja pia na kuwa na diwani aliyechaguliwa kuwa Meya wa Ilala Mh Jerry Slaa hamna chochote anachotusaidia zaidi ya kuonekana kwenye TV na kusafiri kwenda nje ya nchi na amebakia kuleta majibu ya kebehi na dharau kwa wananchi. Na anajiandaa kugombea ubunge 2015 kupitia Magamba. sasa basi CDM tunahitaji kujipanga kwa nguvu kuhakisha tunapata Mgombea mwenye nguvu na utashi wa kuongoza na kutuletea maendeleo jimboni. So vijana tupo tayari kwa mapambano na kutengeneza mtandao wa ushindi 2015, kazi kubwa tuliyonayo ni kufungua matawi jimboni na kupata wanachama wengi. Kwa ushauri na lolote tuwasiliane makamanda kwa ajili ya kuanza kazi rasmi ya kukistawisha chama.
Mkazi wa Ukonga na Mwanachama hai wa CDM-Ukonga Madafu