Uongozi chuo kikuu cha dodoma uache ubabaishaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi chuo kikuu cha dodoma uache ubabaishaji

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mkatanyasi, Apr 20, 2011.

 1. Mkatanyasi

  Mkatanyasi Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
  Lengo la utolewaji wa elimu iliyo bora ni kumsaidia mlengwa kuweza kusimama yeye binafsi bila kuwa tegemezi kwa mtu mwingine ama jamii yake na taifa kiujumla.

  Kuna habari kuwa chuo kikuu cha Dodoma almaarufu UDOM kimekuwa kikiendesha zoezi la utoaji wa elimu kwa vijana wake kwa njia za kibabaishaji.Kwanini ninasema haya? Ninasema hivi kutokana na habari za kuaminika kuwa: WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA CHUONI HAPO WAMEPOKEA TAARIFA KUWA WATAINGIA MADARASANI KWA MUDA WA SIKU KUMI(10) ILI KUWEZA KUFUNDISHWA KOZI (An Introduction To Information Technology) AMBAYO WANAPASWA KUISOMA KWA KIPINDI CHA SEMISTA NZIMA. Sababu zilizotolewa juu ya utaratibu huo ni kuwa chuo hakina walimu wa kozi hiyo hivyo inabidi kuwachukua walimu hao toka vyuo vingine kwa muda.

  SWALI:
  Kama chuo hicho kina uhaba wa walimu wa baadhi ya masomo, kwanini kozi hizo ziliwekwa? Ni nini malengo mahususi ya kuwepo kwa kozi ambazo upatikanaji wa walimu wake ni tatizo?
  Je, ni aina gani ya wataalamu tunaowategemea toka katika chuo hicho na vingine kama vipo vinavyotoa elimu kwa utaratibu huo?
  Je,huu ni mpango wa kutafutiana maisha kwa baadhi yetu kupitia kuwekwa kwa kozi hizo?

  Tunajua kuwa kuna baadhi ya vyuo pia huazima walimu toka vyuo vingine (flying lecturers) ili kuweza kulisongesha mbele gurudumu la taaluma lakini si kwa siku 10 kwa kozi ya semista nzima!

  Inasemekana kuwa wapo wanachuo (mwaka wa pili) ambao waliisoma kozi hiyo kwa kipindi cha semista nzima lakini leo hii hata namna ya kuishika mouse hawawezi na wengine wanakiri kuwa matokeo waliyo nayo katika kozi hiyo ni walimu pekee wanaojua yalipatikana vipi. Hivi, hawa watakaoisoma kwa muda a siku 10 wataondoka na lipi? Huu ni ubabaishaji.

  Hivi,lengo la aina hiyo ya ufundishaji ni kuhakikisha kuwa modules zinakamilika kuonekana zimefundishwa ama wafundishwaji kupata mwanga wa kutosha juu ya kile kilichofundishwa? Hivi katika kipindi hicho cha siku kumi huyu mwanafunzi anasoma kozi moja tu ama kuna kozi zingine pia anazotakiwa kuwa anazisoma kwa wakati huo huo? Watanzania kazi tunayo.

  Kuna haja ya kuwepo kwa chombo mahususi kwa ajili ya kufuatilia utolewaji wa elimu katika vyuo vyetu hivi. Chombo hiki kitaweza saidia kujua kozi ipi ifundishwe kwa wanafunzi wepi, kwa muda gani na kwa malengo yepi. Kama kungekuwa na mtihani wa pamoja kwa vyuo vyote hapa nchini basi kuna baadhi ya vyuo vingefungwa kabisa kwa kuwa na matokeo mabovu kuliko ubovu tunaoujua. Wataalam tutakaowapata kutoka katika vyuo kama hivi ni wataalam wa vyeti pekee na si ujuzi.

  Amka Tanzania, amka mwanafunzi wa kitanzania. Soko la ajira la Afrika Mashariki si lako wewe uliehitimu katika vyuo kama hivi.Utaendelea kuwa mtumwa kiakili mpaka pumzi yako ya mwisho. Tunaamini kuwa wanafunzi mlioko katika taasisi za elimu ya juu mmekombolewa katika elimu ya ufikiri. Itumieni elimu hiyo kupigania haki zenu.

  "EDUCATION IS NOT ONLY POWER BUT THE ABILITY TO USE THE POWER YOU HAVE RECEIVED"
   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nauomba uongozi wa UDOM ujipange sawasawa ili malalamiko yanayotolewa kila mara na wanajamii kuhusu chuo hicho yaweze kupunguzwa kama sio kumalizwa kabisa. Haitashangaza kusilia mwanachuo wa UDOM anatafuta kufundishwa tuition mtaani. Viongozi wakomae... Vinginevyo tutatilia mashaka uwezo wa uongozi wa ndugu zetu hao wateule. Kila mara UDOM! UDOM! UDOM Ah tunaelekea kuchoka sasa.
   
Loading...