Uongo wa madini, ndo huu huu wa gas

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,841
1,843
Mnakumbuka miaka ya mwanzoni mwa 90s, wakati uwekezaji unapigiwa upatu, Na madini ikiwa ni sekta waliyoitolea macho sana mabepari, Viongozi walitembea nchi nzima na kutuambia umaskini wa Tanzania ndo mwisho wake, sekta ya madini itatufikisha katika uchumi wa kati, wakatwambia makampuni yatatujengea hospital za kisasa, shule za kizungu, serikali itakusanya matilioni ya kodi, ajira zitakuwa za kumwaga na longolongo nyiiingi.

Leo hii, madini yanatuingizia hasara kuliko faida, mazingira yako hoi, watanzania wanauawa, mifugo inakufa, na kila aina ya laana hasa katika maeneo ya migodi. Cha ajabu hata serikali haipati hayo matilioni.

Sasa hadithi hiyo imerudiwa sana katika kampeni za 2015, safari hii ilikuwa GAS. kila mtu alisema gas ndo mwokozi wetu, tunaenda katika uchumi wa kati, ajira za kumwaga, mashule yatajengwa, serikali itakusanya matilioni mambo meeengi NA LONGOLONGO NYIINGI.

haijapita hata mwaka mmoja sisikii katika bunge la bajeti jinsi gani wizara zina "align" mipango yao na haya mafanikio ya GAS yaliyosemwa. Siisikii tena GAS ikitamkwa bungeni kama mwokozi, Sioni mipango ya ajira bwelele katika sekta hiyo. Hata waziri wa viwanda sikumsikia akionyesha mpango mkakati wa kutumia GAS kama catalyst ya kufufua viwanda???

HIVI MNAFIKILI SISI WANANCHI HATUNA KUMBUKUMBU, HIVI MNADHANI WATANZANIA NI MALOFA???? CCM NI ILEILE FOR REAL
 
Back
Top Bottom