Uongo na utapeli wa chuo kikuu cha Kampala

charmingboy

Member
Joined
Jun 9, 2015
Posts
29
Reaction score
6
Serikali imewapeleka wanafunzi wa masomo ya afya katika chuo kikuu cha Kampala na kuwatelekeza huko bila msaada na kuendelea kuwakandamiza..

Hivyo wanafunzi wa chuo hicho sasa wanajulikana kama wanasoma nje ya nchi na waziri wa elimu kakiri siku ya jana kwamba ukweli ni chuo cha nje sasa swali ni kwanini wanafunzi waliomba kama ni local undergraduate yaani wanafunzi wa ndani wakapelekwa huko?

Huu ni uzembe wa serikali na wazili husika wa afya pamoja na elimu.na kwanini hawa wanafunzi hupata mikopo na isiwe scholarship kama ni kweli wanafunzi wa nje?

Hii ni kuruhusu mianya ya rushwa.
 
MADAKTARI WATANZANIA WALIOUZWA UGANDA

-Waraka huu ni maalumu kwa dhati kutoka kwa wanafunzi wa fani ya sayansi ya afya kwa kada za udaktari,famasia na maabara waliopo Kampala International University.

Yafuatayo ni malalamiko kutoka kwa wanafunzi ambao tangu mwaka 2011 wamekua wakitafuta suluhu ya matatizo yao kwa bodi na wizara mbalimbali bila kupata ufumbuzi.Matatizo haya ni katika ngazi zote za shahada,stashahada, na astashahada(cheti).

KWA UPANDE WA SHAHADA(BACHELOR DEGREE)

1.TCU -inadahili wanafunzi wa Tanzania kwa mfumo wa CAS na kuwachagua KIU,chuo kinachoongozwa kwa misingi isiyo ya kitanzania kwa kutoa vyeti vya nje ya nchi na kutumia mitaala tofauti na ya kitanzania kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa TCU

2.Kinachotutia woga na wasiwasi zaidi wa wakati mkurugenzi wa TCU katika kikao cha tarehe 15/05/2015 kilichohusisha bodi mbalimbali ikiwemo pharmacy council na NACTE alisema TCU imekisajili chuo na kuruhusu mtaala wa kiganda utumike, lakini kwa upande wa pharmacy council wanashindwa kukisajili chuo katika kada ya ufamadsia ngazi zote sababu kubwa ni mtaala unaotumika. Na hii ni wazi kabisa KIU wanatumia mtaala wa Uganda kwa kada zote za afya lakini sheria inasemaje. Reg. no 47(1) page no 20(TCU regulation) TCU imepuuzia sheria hii kwa KIU.

3.TCU inadahili wanafunzi wa Tanzania kwa mfumo wa CAS local undergraduate kwa maana kwamba tunasoma ndani ya nchi yetu. Lakini tunasikitika kuwa tunauzwa katika chuo cha Uganda.

(a) vyeti vyetu vinatoka Uganda

(b) tunatumia mtaala wa kiganda

(c) hakuna uwezekano wa kusoma chuo kingine chochote hapa nchini mara tukitaka kujiendeleza isipokuwa KIU. Hii ni kwa ngazi zote yaani certificate, diploma na bachelors.

4.TCU ilidahili wanafunzi kupitia CAS katika chuo cha KIU kilichopo Tanzania lakini kinaendeshwa kwa utaratibu wa Uganda na HESLB inatoaje mkopo kwa wanafunzi wa nje ya nchi walioomba kama wa ndani ya nchi?

5.Majukumu ya TCU ni kusimamia vyuo nchini, lakini professional husika zinazofundishwa na ukaguzi wake ni jukumu la bodi husika. Ni kwanini TCU inapitisha na kuruhusu KIU kutumia mitaala tofauti na ya nchi hii?
 
MATATIZO SUGU YANAYOKIKUMBA CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA CHA KAMPALA.

-------

--------Chuo kikuu cha kimataifa cha kampala ni chuo kilichopo maeneo ya Gongo la mboto Dar es salaam, chuo hiki hutoa kozi katika ngazi mbalimbali kama vile astashahada, stashahada na shahada. Kozi zinazotolewa katika chuo hiki ni pamoja na taaluma ya ualimu, biashara, sheria, uandisi na wataalamu wa tiba na afya.

---------Hata hivyo chuo hiki kimekuwa kikikumbwa na matatizo kadha wa kadha hivyo kupelekea wanafunzi katika chuo hicho kuwa na mashaka na elimu inayotolewa katika chuo hicho,

-Miongoni mwa matatizo hayo ni kama ifuatavyo:

1.-Usajili wa kozi za afya.

Pamekuewa na sinto fahamu za muda mrefu juu ya usajili wa kozi za afya kama vile udaktari na upasuaji,famasia na taaluma ya maabara katika bodi husika, toka mwaka 2011 hadi leo na kudhibitika rasmi kwamba kozi hizi hazijasajiliwa na bodi husika mapema mwaka huu ambapo wanafunzi tulipo hoji juu ya jambo hilo katika uongozi wa chuo na baraza la wafamasia na kudhibitika kutoka barua ya bodi hiyo mnamo tarehe 14/4/2015-yenye kumb. N0.AB 300/312/02/20, hata hivyo jambo hili limesababisha taharuki kubwa kwa wanafunzi wa kozi ya tiba na afya hasa wakati wanafunzi wahitimu saba wa ngazi ya astashahada ya famasia waliponyimwa leseni kutoka katika bodi ya famasia kwa kigezo cha kutosajiriwa kwa kozi husika.

-

2.-Mitaala inayotumika kufundishia.

Kumekuwa na utata mkubwa juu ya mitaala inayotumika kufundishia kozi mbalimbali za afya kwani inaonekana kuwa ni tofauti na ile inayotumika katika vyuo vingine.

Kwa mfano-chuo kimekuwa kikifundisha -kozi ijulikanayo kama MPP (MULTI PROFESSIONAL PROGRAMME) ambayo masomo yanayofundishwa huwa ni yale ya sekondari kwa maana ya phizikia,kemia,hesabu,biolojia,kingereza,kompyuta n.k hivyo kusababisha kozi hizi za tiba na afya kuwa ndefu na kuchukua muda mwingi kuliko kawaida kwani mwanafunzi anayesoma udaktari humchukua muda wa miaka 5 na ½ badala ya 5 kamili na

Kwa wanafunzi wa shahada ya famasia huchukua miaka 4 na ½ badala ya 4 kamili pia

Kwa wanafunzi wa shahada ya maabara huchukua miaka 4 na ½ badala ya 3.

Kozi ya MPP (MULTI PROFESSIONAL PROGRAMME) haina umuhimu wowote kwani tayari masomo hayo mwanafunzi anakuwa amekwisha yasoma,kuyafaulu na kuhakikiwa na TCU hivyo husababisha gharama na upotevu wa muda usiokuwa na lazima.

Hata hivyo ziada ya miaka hiyo haitambuliki na bodi ya mikopo ya elimu ya juu hivyo mwanafunzi atalazimika kujilipia -ada na gharama ya miaka hiyo iliyoongezeka.

-

Kwa mtaala wa elimu wa chuo cha -kimataifa kampala mwanafunzi hulazimika kusoma masomo 8-14 kwa semester kitendo ambacho ni kinyume na vyuo vingine.

-

3.-Viwango vya elimu vya wahadhiri na wakufunzi.

Inaonekana kuwa viwango vya elimu vya wahadhiri na wakufunzi wengine katika chuo hiki havikidhi na havina ubora kutokana na kukosa mbinu na ubunifu katika taaluma zao. Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 2012 wanafunzi waligoma kwa sababu ya tatizo hilohilo hivyo tunaomba uchunguzi wa CV na hithibati za wakufunzi hao.

4.-Ukosefu wa vifaa -

(a)-vifaa vya kufundishia

Chuo kina upungufu mkubwa wa nyenzo na zana za kufundishia kama vile ukosefu wa projector,speaker na upungufu mkubwa wa vitabu kwani zipo kozi zingine hufundishwa pasipo kuwepo na kitabu hata kimoja, mfano-kozi ya pharmacognosy, social psychology,microbiology -na pharmaceutics, Kiujumla -maktaba ya chuo haitoshelezi mahitaji ya chuo kutokana na upungufu mkubwa wa vitabu hasa katika upande wa afya.

-

(b)-Vifaa vya maabara

Ubora na utoshelevu wa maabara katika chuo chochote cha afya ndiyo msingi imara kwa mtaalamu wa tiba na afya lakini cha ajabu chuo cha kampala kinazo maabara za kutosha zisizo kuwa na vifaa vinavyomuwezesha mwanafunzi kusoma kwa vitendo.

kutokana na hali hii mwanafunzi husoma masomo ya darasani tu (theory) -pasipo masomo ya vitendo (practical) ya aina yeyote hivyo -kuandaa wataalamu wasiokuwa na ubora wa kuridhisha -ambao kimsingi ndio wanahusika moja kwa moja na uhai wa mtu hii inaweza kuwa ni hatari sana kwa taifa na hata kwa jamii kwa ujumla.
...inaendelea.......
 
5.-Miundombinu hafifu.

Kimuonekano wa nje chuo cha kimataifa cha kampala inaonekana kuwa na majengo mengi na miundombinu bora tofauti na uhahali wa jambo lenyewe kwani miundombinu hii imekuwa ikiendelea kujengwa na kukarabatiwa wakati wanafunzi wakiwa darasani kitu ambacho si sawa kutokana na taratibu za ujenzi katika wizara husika. ----

-

pia Chuo kimekuwa kikiendelea kudahili wanafunzi wengi ukilinganisha na uwepo wa vyumba vya madarasa na rasilimali zilizopo hivyo kusababisha wanafunzi kusoma katika madarasa ambayo hayajakamilika jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa maisha na afya zao kwa ujumla. -

Kwa kuongezea ikumbukwe kwamba sheria ya afya ya jamii ya mwaka 2009 inazuia matumizi ya jengo lolote linaloendelea kujengwa.

-

6.-Kiwango cha ada kinachotozwa.

Ni dhahiri kabisa chuo kikuu cha kimataifa cha kampala kinatoza ada kubwa Zaidi kuliko chuo chochote hapa nchini kwani wanafunzi wa shahada hulipa kiasi cha takribani milioni tatu laki nane (3,800,000) hadi kiasi cha shilingi milioni tisa (9,000,000) kwa wale ambao hawajaletwa na TCU pia cha kushangaza Zaidi mwaka wa kwanza na wa pili hulipa ada tofauti wakati masomo na kozi ni ile ile tulipohoji kuhusu hili wakadai tumeingia chuoni kwa mkataba tofauti pesa ambayo kiuhalali ni kubwa sana ikilinganishwa na uchumi wa nchi na kipato cha mtanzania wa kawaida.

-Pia Chuo cha kimataifa cha kampala ni chuo pekee ambacho wanafunzi wake husoma katika darasa moja na kutumia rasilimali sawa na mbinu za mwalimu mmoja huku wakilipa ada zenye utofauti mkubwa.

-mfano-katika kozi ya MPP (MULTI PROFESSIONAL PROGRAMME) wanafunzi hulipa ada tofauti wakati idadi ya masomo ni sawa na ni Yale Yale tena hayana hata vitendo (practical).

-

Pia kwa mfano-wanafunzi wa ngazi za stashahada na astashahada wapo wanaolipa kiasi cha shilingi milioni tatu laki sita (3,600,000) huku wengine wakilipa kiasi cha shilingi milioni moja laki tisa tu (1,900,000) Pamoja na ulipaji/utozaji wa ada hizo kubwa chuo kimekuwa na matatizo lukuki na utoaji wa elimu ya kiwango cha chini kwa -jamii ya kitanzania na wahitimu wote kwa ujumla ikilinganishwa na vyuo vingine, hivyo basi tungeomba vyombo husika vilitazame jambo -hili cha umakini mkubwa na kulifanyia utekelezaji wa haraka.

-

7.-Mambo mengine yanayokikabiri chuo kikuu cha kimataifa cha kampala ni pamoja na

i.-Sera ya elimu ya chuo kutoeleweka na kubadilikabadilika kila mwaka

v-Kwa mfano-sera ya elimu na mtaala kwa wanafunzi wa ngazi ya stashahada na astashahada.

v-Sera ya udahili wa wanafunzi wanaohamia -katika chuo cha kimataifa cha kampala kutokuwa wazi na kutoeleweka.

v-Utumiaji wa mitaala miwili katika ufundishaji kwa maana ya mtaala wa chuo na muongozo wa NACTE.

v-Wanafunzi wa ngazi ya stashahada na astashahada kuunganishwa katika darasa moja na hivyo kusoma pamoja

------Mfano-diploma mwaka wa tatu (3) kusoma pamoja na certificate mwaka wa pili (2)

-

Hata hivyo mnamo tarehe 10/4/2015-matatizo haya yaliweza kufikishwa katika utawala wa chuo ili kupatiwa ufumbuzi chini ya uangalizi wa OCD wa kituo cha ukonga ndugu SIMBA lakini mwafaka wa matatizo haya haukuweza kufikiwa au kupatikana na hivyo wanafunzi kutaka ufafanuzi Zaidi kutoka katika ofisi za serikali kwa maana ya wizara yenye dhamana na bodi husika. -----------------------------------

-

-Mnamo -tarehe -14/4/2015--tulipokea barua kutoka katika baraza la famasi ikithitibisha kuyapokea madai yetu na hivyo kutegemea kuanza kuyafanyia kazi mapema iwezekanavyo.

-

---------------Serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi mnamo tarehe 16/4/2015-iliweza kufanikiwa kukutana na wanafunzi wakilenga Zaidi usajili wa chuo na kuwataka -wanafunzi wasitishe mgomo -na kuingia madarasani kwani waliahidi kuwa swala hilo limepokelewa na lingeweza kufanyiwa kazi ndani ya muda wa wiki mbili huku wakiwataka wanafunzi wachague wawakilishi watakao saidiana na serikali au bodi husika katika kutatua swala hilo.

Cha ajabu kabla ya kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo -wawakilishi hao pamoja na wale waliokaa katika kikao cha tarehe 10/4/2015-chini ya uangalizi wa kamanda ndugu OCD Simba tulisimamishwa masomo mnamo tarehe 30/4/2015--bila sababu za msingi wala hata ya -kuhojiwa wala kupewa hata nafasi ya kuzungumza hata neno moja -Zaidi ya salamu kisha kusomewa barua za kusimamishwa -chuo mmoja mmoja katika ofisi ya DVC -Mr Abanis -mpaka tarehe 11/8/2015--pindi tutakapoitwa kwenye kamati ya nidhamu hii ikiwa na maana ya kupotezewa muhula mzima wa masomo kabla ya kamati hiyo kutoa maamuzi ya mwisho japo tulichaguliwa na wanafunzi wenzetu kuwawakilisha katika matatizo hayo na kuwaacha wanafunzi wenzetu kushindwa kufuatilia matatizo hayo pamoja na majibu ya bodi ya famasi kuhusu usajili wa chuo kwani yahitaji wawakilishi ambamo ndiyo wale walio ondolewa pia kuingia uwoga na dosari katika uteuzi wa wawakilishi wengine kwani hatima yao kiuhalisia haita kuwa na utofauti na yetu wakibaki kuhangaika na kutetea wenzao warudu chuoni kwani walikuwa wakidai haki sawa na walichaguliwa na wao kuwawakilisha .

Isitoshe mnamo tarehe 29/4/2015-chuo kiliweza kualika vyombo vya habari na kutoa taarifa za kupotosha umma juu ya ukweli wa matatizo yanayokikumba chuo hicho kwa kujisafisha kwa jamii kwa madai kwamba wanafunzi hao waliitwa na kuonywa mara kadhaa wakidai kuwa wengine ni “loiters”-kauli ambayo si ya kweli na -habari hii imetolewa kwa umma na dunia nzima kwa ujumla kupitia gazeti la THE GURDIAN-la tarehe 2/5/2015-lenye ISSN O856 – 5422 ISSUE -NO. 6323-Msemaji wa chuo wa taarifa hiyo ni Afisa masoko na uhusiano ndugu Kenneth Uki.

-Tunaomba vyombo husika -vilishughulikie swala hili kwa umakini huku wanafunzi tulio simamishwa tukiomba turudishwe chuoni -na kuendelea na masomo kama kawaida ili kuepuka upotevu wa muhula mzima.

------
 
Serikali imewapeleka wanafunzi wa masomo ya afya katika chuo kikuu cha Kampala na kuwatelekeza huko bila msaada na kuendelea kuwakandamiza..

Hivyo wanafunzi wa chuo hicho sasa wanajulikana kama wanasoma nje ya nchi na waziri wa elimu kakiri siku ya jana kwamba ukweli ni chuo cha nje sasa swali ni kwanini wanafunzi waliomba kama ni local undergraduate yaani wanafunzi wa ndani wakapelekwa huko?

Huu ni uzembe wa serikali na wazili husika wa afya pamoja na elimu.na kwanini hawa wanafunzi hupata mikopo na isiwe scholarship kama ni kweli wanafunzi wa nje?

Hii ni kuruhusu mianya ya rushwa.

Linapokuja swala zima la elimu,umakini mkubwa unakua unahitajika siku zote. Cha ajabu sote tunashudia jinsi serikali yetu inavyolichukulia hili tatizo la KIU kimzaha mzaha, huku wanaondelea kuumia ni wanafunzi pamoja na familia zao.

Natamani hata raisi ajae awe dikteta ili kwanza adili na hawa vingozi wote wazembe wa awamu ya nne,akianzia na mjomba mwenyewe.one by one wachinjwe hadharani
 
Kuna mtu au watu fulani either TCU au wizarani pale amekula 10% kuhakikisha chuo kinasajiliwa kinyemela

Na huu ni uzembe mkubwa ambao kama mimi ningekuwa president,Kawambwa angenitambua

There must be a chain of command,tuwajibishane hadi tumjue mchawi ni nani,

Lakini pia,now tumeshajua madudu ya hiki chuo,suprisingly,kuna mimtu itaapply tena kwenda pale..Jamani nyie vijana muendao National Service,msiende Kampala,msiende St Joseph,,msipende vyuo vya wahindi ambavyo vipo kibiashara zaidi..Ni bora ukasome diploma Muhimbili au Bugando kuliko kwenda kusoma na HGL pharmacy,Mungu wangu,ataweza kupropose reaction mechanism atengeneze dawa mpya maabara

Siku moja waTZ watachoka na watawala mtajuta
 
hii ni hatari sana kwa taaluma hizi, watakaotoka hapo watakuwa sio wataalamu kamili....kuna haja ya serikali kukagua mitaala ya vyuo vipya na kuhakiki ubora wa majengo na vitendea kazi, pia kujua stability ya hicho chuo kisije kuwa chuo biG cha kusurvive miaka miwili tu na kuanza matatizo.
Nchi hii hiendi bia migomo hilo ni tatizo kubwa sana,hawaanafunzi wamegoma ndio serikali inaona ifuatilie tatz nini...ninalohofia ni kufkuzwa chuo walianzisha mgomo wakati walchokigomeani cha msingi.
 
Kuna mtu au watu fulani either TCU au wizarani pale amekula 10% kuhakikisha chuo kinasajiliwa kinyemela

Na huu ni uzembe mkubwa ambao kama mimi ningekuwa president,Kawambwa angenitambua

There must be a chain of command,tuwajibishane hadi tumjue mchawi ni nani,

Lakini pia,now tumeshajua madudu ya hiki chuo,suprisingly,kuna mimtu itaapply tena kwenda pale..Jamani nyie vijana muendao National Service,msiende Kampala,msiende St Joseph,,msipende vyuo vya wahindi ambavyo vipo kibiashara zaidi..Ni bora ukasome diploma Muhimbili au Bugando kuliko kwenda kusoma na HGL pharmacy,Mungu wangu,ataweza kupropose reaction mechanism atengeneze dawa mpya maabara

Siku moja waTZ watachoka na watawala mtajuta

Huyo kwenye bluu ndio waziri wa elimu ya juu? maana kuna waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi na wazara ya elimu ya juu.
 
Regulatory and supervisory bodies wako wapi? Hii ni fedheha kwa nchi!.
 
Unajua sometime wanafunzi wa kiu mnatuchanga, waziri na jop lake ikiwemo TCU na NACTE wote wa mekuja pale nakusema matatizo wanayatambua na chuo kuhusu kusajiliwa kimesajiliwa na tcu.

waziri wa elimu akasema atawasiliana na waziri wa Afya watatue huo mzozo sasa mie nashangaa kuhusu complain then kwamba serikali wafanye nini sasa?

sie hapo chuoni atupo Lakini vyombo vya habari tunaona tena waziri kasema mitaala ya kufundishia kuanzia wanafunzi wapya watatumia mitaala ya local undergraduate na sio hii ya sasa,embu tujuzeni wanafunzi waziri kaongopa?wasi wasi wenu nini sasa vijana?

tulieni na kusubiri utekelezaji wakizingua mnaingia barabarani kama kawa.
 
Jamani hizi sio university za maana , ni hiyo njaa tu na lack of control. Vyuo vya kata!
 
Serikali pamoja na chuo kikuu cha kampala kitivo cha afya washirikiana kunipotezea ndoto zangu;

Ndugu watanzania,leo naandika hivi nikiwa na majozi pale ninapoona wanasiasa wakishindana kwa jukwaa kwa sera zenye mashiko kwa watanzania lakini hazifanyiwagi kazi.Hakika sera ya maisha bora inapita lakini ugumu wa maisha bado unazidisha makali yake na mfuko wa taifa hili ukiendelea kutumika na wachache kwa manufaa yao.

Mimi nilikuwa mwanafunzi wa udaktari chuo kikuu cha kampala dar .Kwa sasa ndoto hizo zimefutika na kuharibiwa na viongozi kadhaa wa nchi hii.Hakika sita sahau kauli toka kwa kiongozi mmoja wa tume ya elimu ya juu aliposema siyo lazima tuwe madaktari hata kama tumesomea udaktari maneno haya dhairi yalionesha kwamba wapo tayari kutupotezea muda huku wakijua fika kwamba elimu tunayopata pale haina tija kwa wananchi wapenda maendeleo watanzania.

Napenda itambulike wazi kwamba sisi wanafunzi wa kampala university hatujarudi chuoni na hatutarudi mpaka chuo chetu katika kitivo cha afya kipate usajiri ulio kamili.Napenda tanzania itambue kwamba wanafunzi wanaosoma pale si madaktari bora kwa kutoa huduma ya afya tanzania na duniani kote kwa hiyo chuo hicho hakipo kwa ajili ya kutoa elimu iliyo bora yenye tija kwa taifa hili.4

Kunaonekana kuwa na siri mzito sana ya mizunguko ya fedha isiyorasmi katika chuo hiki .Mh waziri wa elimu aliwasiri chuoni hapa na kusema kwamaba chuo hicho kimesajiliwa kama chuo cha nje na kutokana na pointi hiyo chuo hiki hakikupaswa kuingiliwa na sheria zozote za nchi hii ikiwa kama kuletewa wanafunzi kwa kupitia central adimission systeme,kupata loans kutoka katika board ya mikopo ukijaribu kuchanganua hiyo taarifa imebeba maana kubwa sana nyuma yake

SIRI YA JAMBO HILI NI SAWA NA YALE YOTE YA UFISADI(ESCROW,RICHMOND N.K)
viongozi hawa wametumia mwanya huo wa kukipa chuo kisicho na tija mikopo lakini tukitafakari kiundani si lengo kamili kwao kusaidia wananchi bali lengo linaloonekana ni kutafuta mwanya wa kuchota pesa iliyo kule hazina ya bodi ya mikopo (HESLB) kwa hiyo kwa mbinu ya kufanya hivyo inaonekana kusudio lake ni kupata pesa toka serikalini kwa matumizi yao binafsi.

Ndugu watanzania mnaibia nmi pia naibiwa.Na hii ndio sababu iliyofanya viongozi kadhaa kutetea chuo hiki kwa nguvu kali ya kutumia vyombo vya dola yaani polisi wa pale gongo la mboto yanini mapambano ya hoja yakatumia nguvu kubwa hivi mpaka wananchi wa eneo lile kushtushwa na usalama wao,kwa nini polisi wanatumika mpaka wanadiliki kufuata wanafunzi hosteli kwao na kuwakamata kila wanapo waona hii ni nguvu ambayo bado siwezi itathmini imetokea kwa nini.sasa wanadiriki kusema yule anaekataa kusajili atawajibishwa kwa nini awajibishwe kama anatetea uhai na maisha ya watanzania hapa panaonekana wazi kuna maslahi binafsi wanayatetea.

Ukweli ni kwamba watanzania Tuamke tuikatae hali hii sisi wanafunzi wa kiu wameamua kutujengea maisha bora kwa kutunyima elimu bora tuliyokusudia na mpaka sasa tupo mtaani huku tume ya vyuo vikuu kupitia mkurugenzi wake wakitoa taarifa kwamba sisi wanafunzi tuliopo nje ya chuo ni kikundi tuu cha vijana ambao hawapendi kusoma naamini kwamba zambi ya hili itajibiwa tuu maana jumla ya wanafunzi tuliopo nje kwa sensa ya mwezi uliopita tulikuwa wanafunzi 362 je hawa wote hawapendi kusoma?

Tunapata taarifa nyingi sana kwamba wanatoa matangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu nafasi za masomo NAWAAMBIA WATANZANIA MTAIBIWA KUWENI MAKINI NA VYUO HIVI.NA MFUATILIE.

ukweli nina mabo mengi sana ya kusema lakini naomba niishie hapa.NA NITOE USHAULI WANGU KWAMBA WANAFUNZI MLIOMALIZA KUWENI MAKINI NA VYUO HIVYO KAMPALA NA ST JOSEPH ARUSHA FUATILIENI MSIKURUPUKE SISI TUMEPITIA HUKO MPAKA SASA MAISHA YETU WAMEYAALIBU.AHSANTENI SANA.
 
...pole sana wanachuo!
Bao la mkono kila idara!
 
Khaa!! What is your point? Naona umeandika hovyohovyo tu. Au ndiyo lugha za madaktari wanafunzi? Nauliza tu :glasses-nerdy:
 
Akija kutoa maelezo yanayoelewaka naomba uniite.!
 
kumbe chuo chenyewe KIU! kwa maoni yangu nninachojua ile ni kama business entity tu! I am so doubtfully hata na elimu inayotolewa kwenye hicho chuo! kwanza kina hata huo usajili! Tafadhali mliopo serekalini futilieni ubora wa taaluma inayptolewa pale kuliokoa taifa hili.

Serikali pamoja na chuo kikuu cha kampala kitivo cha afya washirikiana kunipotezea ndoto zangu;

Ndugu watanzania,leo naandika hivi nikiwa na majozi pale ninapoona wanasiasa wakishindana kwa jukwaa kwa sera zenye mashiko kwa watanzania lakini hazifanyiwagi kazi.Hakika sera ya maisha bora inapita lakini ugumu wa maisha bado unazidisha makali yake na mfuko wa taifa hili ukiendelea kutumika na wachache kwa manufaa yao.

Mimi nilikuwa mwanafunzi wa udaktari chuo kikuu cha kampala dar .Kwa sasa ndoto hizo zimefutika na kuharibiwa na viongozi kadhaa wa nchi hii.Hakika sita sahau kauli toka kwa kiongozi mmoja wa tume ya elimu ya juu aliposema siyo lazima tuwe madaktari hata kama tumesomea udaktari maneno haya dhairi yalionesha kwamba wapo tayari kutupotezea muda huku wakijua fika kwamba elimu tunayopata pale haina tija kwa wananchi wapenda maendeleo watanzania.

Napenda itambulike wazi kwamba sisi wanafunzi wa kampala university hatujarudi chuoni na hatutarudi mpaka chuo chetu katika kitivo cha afya kipate usajiri ulio kamili.Napenda tanzania itambue kwamba wanafunzi wanaosoma pale si madaktari bora kwa kutoa huduma ya afya tanzania na duniani kote kwa hiyo chuo hicho hakipo kwa ajili ya kutoa elimu iliyo bora yenye tija kwa taifa hili.4

Kunaonekana kuwa na siri mzito sana ya mizunguko ya fedha isiyorasmi katika chuo hiki .Mh waziri wa elimu aliwasiri chuoni hapa na kusema kwamaba chuo hicho kimesajiliwa kama chuo cha nje na kutokana na pointi hiyo chuo hiki hakikupaswa kuingiliwa na sheria zozote za nchi hii ikiwa kama kuletewa wanafunzi kwa kupitia central adimission systeme,kupata loans kutoka katika board ya mikopo ukijaribu kuchanganua hiyo taarifa imebeba maana kubwa sana nyuma yake

SIRI YA JAMBO HILI NI SAWA NA YALE YOTE YA UFISADI(ESCROW,RICHMOND N.K)
viongozi hawa wametumia mwanya huo wa kukipa chuo kisicho na tija mikopo lakini tukitafakari kiundani si lengo kamili kwao kusaidia wananchi bali lengo linaloonekana ni kutafuta mwanya wa kuchota pesa iliyo kule hazina ya bodi ya mikopo (HESLB) kwa hiyo kwa mbinu ya kufanya hivyo inaonekana kusudio lake ni kupata pesa toka serikalini kwa matumizi yao binafsi.

Ndugu watanzania mnaibia nmi pia naibiwa.Na hii ndio sababu iliyofanya viongozi kadhaa kutetea chuo hiki kwa nguvu kali ya kutumia vyombo vya dola yaani polisi wa pale gongo la mboto yanini mapambano ya hoja yakatumia nguvu kubwa hivi mpaka wananchi wa eneo lile kushtushwa na usalama wao,kwa nini polisi wanatumika mpaka wanadiliki kufuata wanafunzi hosteli kwao na kuwakamata kila wanapo waona hii ni nguvu ambayo bado siwezi itathmini imetokea kwa nini.sasa wanadiriki kusema yule anaekataa kusajili atawajibishwa kwa nini awajibishwe kama anatetea uhai na maisha ya watanzania hapa panaonekana wazi kuna maslahi binafsi wanayatetea.

Ukweli ni kwamba watanzania Tuamke tuikatae hali hii sisi wanafunzi wa kiu wameamua kutujengea maisha bora kwa kutunyima elimu bora tuliyokusudia na mpaka sasa tupo mtaani huku tume ya vyuo vikuu kupitia mkurugenzi wake wakitoa taarifa kwamba sisi wanafunzi tuliopo nje ya chuo ni kikundi tuu cha vijana ambao hawapendi kusoma naamini kwamba zambi ya hili itajibiwa tuu maana jumla ya wanafunzi tuliopo nje kwa sensa ya mwezi uliopita tulikuwa wanafunzi 362 je hawa wote hawapendi kusoma?

Tunapata taarifa nyingi sana kwamba wanatoa matangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu nafasi za masomo NAWAAMBIA WATANZANIA MTAIBIWA KUWENI MAKINI NA VYUO HIVI.NA MFUATILIE.

ukweli nina mabo mengi sana ya kusema lakini naomba niishie hapa.NA NITOE USHAULI WANGU KWAMBA WANAFUNZI MLIOMALIZA KUWENI MAKINI NA VYUO HIVYO KAMPALA NA ST JOSEPH ARUSHA FUATILIENI MSIKURUPUKE SISI TUMEPITIA HUKO MPAKA SASA MAISHA YETU WAMEYAALIBU.AHSANTENI SANA.
 
DUH,,,,,SASA MWAKA HUU KIMERUHUSIWAJE KUFANYA USAILI.
 
Back
Top Bottom