Uongo — Dhambi tuliyoizoea inayoangamiza taifa letu

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
8,036
Reaction score
20,031
Wengi tunauchukulia uongo kama ujanja wa kuishi au kutawala. Tunadanganya ili tupate nafasi, kupenya kwenye ulaji, kujiokoa, au kuonekana wema. Lakini taratibu, bila kujua, tunajenga taifa linaloharibiwa na uongo wa kila siku.

Biblia inasema nini juu ya uongo?

“Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana; bali wafanyao kweli wamfurahisha.”— Mithali 12:22.

Uongo ni chukizo, sio tabia ya mtu anayetaka maendeleo ya jamii. Huu ni msingi wa maadili ya taifa lolote linalotaka kusimama imara.

Amri ya 9: Usitoe ushuhuda wa uongo juu ya jirani yako.” Uongo unaangamiza haki — na bila haki, taifa hubaki dhaifu.

Qur’an inasema nini juu ya uongo?

jiepusheni na kauli ya uongo.— Qur’an 22:30

Uongo ni sumu ya maadili. Qur’an inaona uongo kama tabia inayovunja uaminifu kati ya watu — nguzo muhimu ya taifa lolote.

Qur’an 16:105, Hakika wanaozua uongo… ndio waongo. Uongo unapozoeleka, watu wanapoteza hofu ya Mungu na heshima ya taifa.

Uongo umegeuzwa kuwa njia ya kupata haki, njia ya kupata kazi, njia ya kushinda, njia ya kusurvive, Lakini kwa hakika, ndio chanzo cha kuporomoka kwa maadili, udumavu wa maendeleo, na kuchelewa kwa ndoto za taifa letu.

Taifa lisilosema kweli haliwezi kujenga maendeleo ya kweli.
Uongo unavunja imani na bila imani hakuna taifa.
Kweli inajenga msingi wa haki bila haki hakuna amani ya kudumu.

Je, tatizo la uongo lilianza wapi je tuliweka misingi taifa kwa uongo na kufanya uongo kuwa sehemu ya maisha yetu

Na je, kama taifa, tuko tayari kujitazama kwenye kioo na kusema tumefika hapa kwa sababu tulikubali uongo uwe sehemu ya mfumo wetu.
 
Biblia methali 29 .12
Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.
 
Kuna dhambi nyingine ambayo nyerere anaongelea sana. Dhambi hii ni ile ya kujifanya hamna tatizo na kulipotezea kufhani nalo litapotea
 
Kabisa upo sahihi Sijui tufanyaje kuondo hizo vitu kwa viongozi wetu..
 
Mabadiliko ya fikra lazima yasukumwe, ifikie mahali uongo uonekane kama ukimwi

Kwenye hili hao waliopo sahiz itakuwa ngumu lakin with enough force watabaki hawana jinsi
 
Kabisa kabisa
 
Back
Top Bottom