Uoga wa vijana ni neema kwa matapeli

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,221
22,295
UOGA WA VIJANA NI NEEMA KWA MATAPELI.

Wakuu natumaini mko poa.

Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi. Kwa pamoja mjibu CHAMA KIENDELEE. Leo nimeona nitoe maoni yangu kuhusu mambo ya biashara na ujasiriamali kwa sababu kuna mambo hayako sawa.

Kwanza niwapongeze vijana wote wa kitanzania mnaopambana kuushinda umaskini. Hakika ninyi ni baraka katika nchi. Changamoto iliyopo kwa wengi ni UOGA. Hili jambo limekuwa likizima ndoto za vijana wengi sana. Uoga bado ni tatizo kubwa. Vijana wana akili nyingi na wengi kwa sasa wamepita shule ila haziwasaidii na kujikuta kijana mtu mzima analishwa na mama yake mponda kokoto. Uoga umeleta athari nyingi sana ila kwa sasa uoga una mchango mkubwa sana kwenye kuimarisha UTAPELI. Hakika matapeli wanatumia fursa vizuri.

Ikumbukwe kwa nchi yetu ilivyo tunaposema biashara basi automatically tunamaanisha kununua na kuuza. Hii iko hivi kutokana na ukosefu wa viwanda na elimu duni ya kumwezesha mtu kuwa mbunifu hivyo kuanzisha kitu tofauti na uchuuzi. Mitandaoni tunaona wengi wanaagiza mizigo China na kwingineko na kuja kuuza nchini. Sasa je hawa matapeli wananeemeka vipi? Jibu ni kwamba kutokana na uoga wa vijana wengi kwenye kuthubutu kwenda mstari wa mbele na kufanya mambo wenyewe huamua kutumia madalali kuwafanyia mambo yao. Baadhi ya madalali hufanya kwa weledi lakini wengine huishia kutapeli na kuzima ndoto za vijana.

Binafsi naona vijana wengi ni uoga wao tu unawapelekea kutapeliwa. Teknolojia imerahisisha mambo mengi mno. Mitandaoni kuna sites nyingi sana za kuuza vitu ambapo ni wewe mwenyewe kuchagua ununulie wapi. Namna za kufanya malipo zipo kibao. Wasafirishaji nao hawako nyuma ni kiasi cha kuwaunganisha na muuzaji na wao kukutumia mzigo wako. Sasa huu uoga wa mtu kuamua kutumia dalali ni wa kazi gani? Unashindwa kuingia Alibaba ukaagiza kitu chako na kuwaunganisha na makampuni ya usafirishaji ukatumiwa mzigo? Hiyo smartphone uliyo nayo inakusaidiaje?

Ukiingia Instagram kuna malalmiko mengi mno ya watu kudhulumiwa pesa zao au kutotumiwa mzigo uliokamilika. Vijana tuache upuuzi wa kutumia madalali kwenye kila kitu wakati mtandaoni taarifa za kila kitu kipo.

Asanteni sana. Mbarikiwe
 
Hadi wale wauza Simu mixer sabuni wamerudi kwa kasi hapo ubungo daraja la kijazi, japo population imepungua ila wapo kama 7 hivi, jana mmoja nikamuuliza bado mnawapata wajinga mbona huu ni wizi wa zamani sana, akasema wajinga hawaishi wakiona hii smartphone wanaingia tamaa ,simu ya laki+ anataka kupata kwa 30000.....
 
None of the two
share na vijana knowledge na skills watu wajifunze na sio kulaumu na kukashifu watu tu kuto kuwa nacho leo haimaanishi maisha yameisha kesho unaweza kupata kuliko kulaumina bora kushauriana kama vijana nakutiana moyo tu. wengi wanalazimishwa kusoma vitu havina faida kweny jamii ya ss kutokana wamefaulu na mikopo ila wagejuaa kwamba mamb ya mtaani hayana formula naamini watu wange acha toka f4 kusoma
yan ss vijana ndio tunachuki sn wenyew kwa wenyw hasa mtu akipata kitu anaona wezake kama hawajielewi kabisa
kila mtu anafight sn apate maisha bac tu.

mkuu au umetumwa na chama nini.
 
share na vijana knowledge na skills watu wajifunze na sio kulaumu na kukashifu watu tu kuto kuwa nacho leo haimaanishi maisha yameisha kesho unaweza kupata kuliko kulaumina bora kushauriana kama vijana nakutiana moyo tu. wengi wanalazimishwa kusoma vitu havina faida kweny jamii ya ss kutokana wamefaulu na mikopo ila wagejuaa kwamba mamb ya mtaani hayana formula naamini watu wange acha toka f4 kusoma
yan ss vijana ndio tunachuki sn wenyew kwa wenyw hasa mtu akipata kitu anaona wezake kama hawajielewi kabisa
kila mtu anafight sn apate maisha bac tu.

mkuu au umetumwa na chama nini.
Ninapenda wengi kama sio wote tufanikiwe ndo maana nimeandika huu uzi. Na hakuna nilipokashifu mtu. Uoga ni jambo la kuamua tu kuacha na wala sio kilema cha maisha. Na uzi huu haujalenga wale ambao hawajui chochote. Hao ni case nyingine. Hapa nimelenga wale wanaojua michakato yote ila waoga kutenda. Ambaye hajui lazima naye awe na kiu ya kutaka taarifa sahihi na maarifa mapya. Usitegemee ukae tu huulizi mtu akaota huyu hajui kitu fulani. CCM haijanituma kuandika huu uzi. Ni uamuzi wangu binafsi.
 
Back
Top Bottom