Unywaji Wa maji kupita kiasi.

Mrs milas

Senior Member
Mar 23, 2017
100
90
Wasalam,

Madaktari naomba msaada, nimekuwa nakunywa maji na kukojoa kila wakati. Kiu inakuwa Kali kiasi nahisi kuchanganyikiwa midomo inakuwa kama imekauka hivi na dawa pekee ni maji, nakunywa maji hadi Lita 6 kwa siku. Nikinywa maji nahisi kabisa tumbo limejaa lakini bado kiu inakuja Kali.

Ratiba ya maji kama Inavyopendekezwa na wadau humu ndani nashindwa kabisa kuifuata, huwa naanza vizuri asubuhi tu kwa kunywa glasi moja ya maji ya moto, Mara baada ya kupata chai ndio shida inaanza hapo, nitakunywa maji mfuliluzo hadi mida ya lunch nikimaliza kula nakunywa maji endlessly hadi jioni na Nikila chakula cha jioni ni kiu Kali ya maji , nimekuwa nikilala SAA 6-7 sababu ya usumbufu Wa kukojoa na nahitajika kuamka kila wakati,

Nahisi nakojoa kupita kiasi cha maji ninayo kunywa... Hili lilianza 2013 lakini nilipima sukari na kukutwa sina, nimebahatika kupata watoto wawili, kipindi chote cha ujauziti huwa sinywi maji na wala huwa sina kiu km sasa.

Nawaombeni msaada nimetoa hayo maelezo ili muweze kunishauri vizuri. Asanteni.
 
Hali hiyo si yakawaida... Tembelea vituo vya afya kwa vipimo zaidi...

Mimi nakushairi ubebe ujauzito tena
 
Hali hiyo si yakawaida... Tembelea vituo vya afya kwa vipimo zaidi...

Mimi nakushairi ubebe ujauzito tena
Mkuu,nitaenda hospitali ya hindu mandal Leo jioni, nadhani nitapata Huduma nzuri.

Jamani kubeba ujauzito tena hapana nimefikia "population momentum"
 
Hiyo hali hata mimi inanikuta mpaka sasa hivi..nimekuwa mlevi wa maji kabisa na ninashindwa kuacha...kila siku lazima ninywe maji kama lita 5-7...ila najaribu kupunguza kipimo nashindwa
 
Hali hii si ya kawaida, hebu wenye msaada juu hili mtusaidie tujue.
Kitu kingine umenikumbusha Mimi mwenyewe mwili wangu hauna uwezo wa kustahimili maji hata glass moja lazima nikojoe tu, haijalishi ninasweat au vip, bado maji huwa hayakai mwiliini, na kwa upande wangu nisaidieni, wakuu
 
Hiyo hali hata mimi inanikuta mpaka sasa hivi..nimekuwa mlevi wa maji kabisa na ninashindwa kuacha...kila siku lazima ninywe maji kama lita 5-7...ila najaribu kupunguza kipimo nashindwa
Mkuu twende hospitali kwa msaada zaidi, hata hivo Leo jioni nkiwahi naenda hospitali, nikichelewa kesho mbio asubuhi.
 
Back
Top Bottom