Hivi kwanini nizidi kupenda nchi yangu kwa lipi jema kama sisi huku jimboni kwetu Nyasa tulivyosahaulika toka uhuru mpaka leo kila sekta ni shida.
Nikianza na barabara hazipitiki utadhani wanyama ndio huishi huku.
Huduma za afya nazo shida, ndugu zetu hufa njiani kuelekea wilaya jirani ya Mbinga kupatiwa huduma ambapo barabara mpaka ufike huko Mbinga ni shida.
WanaJamiiForums tunaomba mtusaidie kuwakumbusha viongozi wetu juu ya ahadi zao vinginevyo unyanyasaji huu sio mzuri na sisi ni binadamu jamani. Ndege zinanunuliwa, treni za mwendo kasi zinaandaliwa, kwanini sisi huku Nyasa tusahaulike?