Katika Maandiko Matakatifu, UKOMA kama ulivyo UKIMWI ulikuwa ugonjwa wa kuambukiza usio na tiba wagonjwa walitenngwa. Tusome Mambo ya Walawi 13:45-46.
Mtu mwenye ukoma aliye na pigo ndani yake, atavaa nguo zilizoraruka, na nywele timutimu; na ataufunika mdomo wake wa juu na kusema, "Ni najisi, ni najisi" Kwa siku zote ambazo pigo litakuwa ndani yake atakuwa najisi, ataishi kwa upweke katika makazi yake, nje ya kambi.