Unyama watokea kagera

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Majambazi yateka magari 18 ya mizigo, abiria wilayani Biharamulo jana. Abiria wapigwa, waporwa fedha, simu. Polisi yaendesha operesheni kuwasaka.
 
Poleni abiria,,, hawa majambazi ni polisi wenyewe!!!!!!!!!
Tena kituo cha nyakanazi ni balaa wasijue kama una hela hutafika unakokwenda haijalishi uko kwa bus au private car..
Kuna siku nilitoka kahama kwenda bujumbura na gari kulikuwa na mtu ana hela kilichotupata sina hamu!!!
 


Funguka mkuu!
 
hivi lini haya madhila yataisha jamani, poleni sana mliodhalilisha na hao mafirauni
 
mmewatimua DRC mnategemea nini?
 
Majambazi yateka magari 18 ya mizigo, abiria wilayani Biharamulo jana. Abiria wapigwa, waporwa fedha, simu. Polisi yaendesha operesheni kuwasaka.

...wahamiaji haramu si walifukuzwa wote!
maana ndiyo waliokuwa wanateka na kupora...!
 
Wameanza kutafuta pesa kwa ajili ya sikukuu zinazokuja na Karo kwa ajili ya watoto wao January mwakani. Jamani wanaotumia barabara hiyo, kuweni makini kusafiri siku ya alhamisi kwani ni siku ya Mnada wa Ng'ombe Lusahunga na ijumaa ni siku ya mnada Nyakahura Minzani(Kama sikosei) so kutekwa ni njenje!!!!
 
Wameanza tena hapo utasikia wakimbizi ndio majambazi......
 

Hata bila ya hiyo minada,,, j5 kuna gari imetekwa kupita kabanga kidogo.
 

Hapo munzani ni pabaya sana polisi wanajifanya kulinda kumbe wanachukua details za wenye hela.. ili huko mbele wawateke!
 
safi kabisa tugawane umaskini hiyo....ila wangekuwa wanaenda kuwateka na kuwapora wabunge na mawaziri pale dodoma kipindi cha bunge ingekuwa powa zaidi
 
... "tutakuja ambiwa kuwa ni wanaCHAMA wa..., ndiyo waliofanya uporaji"

C hukua C hako M apema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…