Hili jambo linaonesha kuna mapana ndani yake ambapo, ama waTZ hatupewi taarifa sahihi za kwanini siri-kali haiwi aggressive kwenye jambo kama hilo ilhali ushahidi halali upo au pengine kuna malalamiko ya Wamsumbiji kunyanyasika ndani ya TZ ambayo na wao wanalalamikia nchi kwao bila sisi kusikia.
Zipo kesi za wageni kukamatwa na watu wa uhamiaji, na baada ya kuonesha vibali vyote halali, walipewa kesi ya kukutwa na BANGE na wengine kuambiwa hawaruhusiwi kufanya kazi hapa ilhali wamekamatwa wakiwa kwa mama lishe wanajipatia mlo wa siku. Wanafikishwa mahakamani na kuishia kulipa milioni moja tzs.
Nitoe mfano mdogo: Mji wa Dar kwa sasa askari wa barabarani wamepewa zile mashine za EFD, akikusimamisha na kukuta na kosa basi utakatiwa tiketi yako ukalipe faini. Tatizo ni hili; Nimesimamishwa na huyu askari mwenye mashine, cha kwanza anakwambia, 'naomba leseni yako nikague', unampa, hapo sasa anaizuia na kuanza kutafuta makosa. Lakini hata kama hakuna kosa, ano uwezo wa kukuandikia tiketi kwakuwa tayari anayo namba ya leseni yako. Sasa ukubali kuipokea tiketi au ukatae, mwisho wa siku utakutana na ile PENALTY siku ya ku-renew leseni yako TRA. Sina elimu ni vipi nitaipinga faini hiyo kama kosa nimebambikwa? Zamani ilikuwa unagoma kusaini au unasaini kwenye kutokukubali kosa kisha unaenda mahakamani, leo unafanyaje kupata haki ilhali umeshaandikiwa?
Kwa mfano huo tu ambao umenikuta wiki iliyopita, kama mgeni akifanyiwa hivi na ilhali anajua anatendewa ndivyo sivyo, hawezi kulalamika nchini kwao? Wakiwa wengi wanalalamikia jambo moja, hawatahemkwa kama sisi sasa hivi? Nini kitafuata?
Pia, wengi wanakimbilia kule kwaajili ya kutafuta maisha, shughuli zitajazwo kuwa wengi wanazifuata kule ni pamoja na uchimbaji madini na mama lishe. Hivi ni kweli kuna haja ya kuikimbia nchi yenye kila aina ya madini kwenye ardhi kwenda kuteseka ugenini? Hatuna migodi? Kama issue ni kutotendewa sawa na watawala wetu nyumbani, ugenini ndio utathaminiwa kuliko mzawa?
Tutafute taarifa za kina kabisa ili tujiridhishe pasi na shaka; ni sababu zipi zipelekeazo ndugu zetu wanyanyaswe ilhali wana vibali halali. Kisha tuanzie hapo ili tusijejuta. Kwanini sasa?