Wakati Kamati ya Bunge ilipotembelea kiwanda cha TANELEC walielezwa na uongozi wa kiwanda kuwa TANESCO wamenunua tranformers chache kutoka kiwandani hapo na idadi kubwa za transformers zimekuwa zikinunuliwa kutoka nje ya nchi. Mimi sijajua ni sababu gani iliyopelekea Tanesco kununua transformers kutoka nje ya nchi huku tukiwa na kiwanda chetu kinachotoa bidhaa zenye ubora kabisa. Kwa vile suala la viwanda lilikuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 na limesisitizwa sana na Mhe.Magufuli sasa ni wakati muafaka Tannesco waache MARA MOJA kununua transformers kutoka nje ya nchi na badala yake wanunue kutoka kiwanda cha Tanelec.