Alafu mafundi wengi wanaziogopa za promotion, hivyo ahakikishe huyo fundi yupo safi vinginevyo hawataiweza, binafsi me mwenyewe nilinunua simu TECNO H6 nilisahau password kilichotokea nikapeleka kwa fundi baada ya kujaribu kufanya trouble shooting nikashindwa ile ya (ku-hold power off na sehemu ya kuongezea sauti ili baadae una reboot). Mie ile simu nilikuwa nimeinunua dukani kabisa na nikawa naitumia kwa line ya airtel na voda ila niligundua baadae ile simu muuzaji anazinunua za promotion alafu anazi-unlock na kuziweka dukani kwa kuwa ilikuwa ina apps ya tigo pesa.
Nikaipeleka kwa fundi akaleta issue kwamba itabidi arudishie file lake na analo wakakomaa nayo wakafanikiwa ila kichekesho ikawa sasa ili line nyingine ifanye kazi lazima uweke tigo (hapa ile hofu yangu ya awali ya kwamba simu ya promotion ndipo nilijua ipo kweli maana walivuruga system kiasi kwamba ikaua IMEI namba na nilikuwa mkoa). Nilivyoenda Dar nikapeleka ofisi za TECNO ila tena ikaonekana kama nimeiiba maana walinitaka receipt kwa kuwa ilikuwa imeua IMEI but baadae wakaishughulia ikatengemaa na kuirudisha ktk kiwango chake original na ililoga of course mie ndo niliisababisha nikaipeleka tena wakairekebisha na inadunda.
Kikubwa kama ana receipt au kama hana ila ana uhakika ni simu original na haijaibiwa popote, aipeleke ofisi ya TECNO watamtengenezea bure (ila kama yupo Dar na simu kikubwa iwe imenunuliwa ndani ya mwaka na iwe haijawahi kuchokonolewa na mafundi wengine). Jamaa wapo opposite na police post Msimbazi utaona ghorofa lina bango la TECNO juu akipanda ngazi juu anawapa wanamrekebishia bure kabisa