Ungesubiri kidogo mh. Lowasa na kuwa kichwa ngumu heshima yako ingebaki pale pale


sammosses

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
1,344
Points
1,500
sammosses

sammosses

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
1,344 1,500
E Lowasa ni kiongozi mvumilivu na mwenye kustahili tuzo ya mwanasiasa mvumilivu kuliko hata mzee Marecela.Ni mvumilivu kutokana na siasa za maji taka ambazo zimeshamiri katika nchi yetu.Ni msikivu ndiyo maana hakutaka kupoteza muda wa kurumbana na watu kwenye vyombo vya habari.

E L si mtu wa mchezo mchezo ambaye una weza kumbeza kirahisi kutokana na influence aliyo nayo.Umakini na uthubutu wake wa kufanya maamuzi magumu ndiyo kitu pekee kilichompelekea mheshimiwa huyu kufanya maamuzi magumu ya kujiuzuru akiwa ni mfuasi mahiri wa siasa za uwajibikaji.

Aliamua kuonyesha njia ili kuinusuru serikali pamoja na kuwa serikali ilishindwa kuudhibitishia umma ushiriki wake wa moja kwa moja kutokana na tuhuma zilizo mkabili.Serikali na chama chake kilicho shika dola kimeendelea kuonyesha udhaifu wake kwa kupambana na mtu mmoja aliye shupavu na kuzidi kudhihirisha udhaifu wa CCM na serikali yake.

Tuhuma tu ndani ya serikali ambayo aliisimamia haitoshi kuwaaminisha Watanzania kuwa mtu huyu ni mchafu bila kupamabanua uchafu wake ni upi ilhali akiendelea kupewa nyadhifa nzito ndani ya bunge.

Kwa kitendo chake cha kuchaguliwa na wananchi wanachama wa CCM wilayani Monduli kwa kura nyingi na kuwa MNEC kinadhihirisha umakini wake na ujasiri wake ambao laiti kama angekuwa mtu dhaifu tunge msahau kwenye ulimwengu wa siasa.

Ataendelea kukitesa chama chake mpaka pale chama kitapokuwa na ubavu wa kumweleza wazi mwenyekiti wake kuwa yeye ndiye gamba linalo stahili kuvuliwa.Alisema ndani ya NEC,hakuna alichokifanya katika sakata la Richmond bila kupata baraka za rais wake ambaye kama inavyotamkwa kwenye katiba ya JMT kuwa waziri mkuu atawajibika kwa rais na kutekeleza yale atayoamriwa na rais wake.

Amelizungumza hili kwenye NEC M/Kiti amekaa kimya,wajumbe nao halikadhalika.Hatujaona chama wala tamko la vikao halali vya chama vikitekelezwa zaidi ya kutelekezwa kwa maazimio ya kujivua gamba.Sumaye alihoji,ikithibitika wanao mchafua mh Lowasa kinyume na taratibu za chama,M/Kiti alipata kigugumizi na kusema watachukuliwa hatua za kinidhamu,lakini mpaka sasa hatujasikia lolote zaidi ya kuiweka kabatini kauli mbiu yao ya kujivua gamba na kushindwa kuwawajibisha wale wote waliotakiwa kujivua gamba.

Mantiki hasa ya kuandika mada hii ni kumlaumu mh. Lowasa kwa kushindwa kuwa mvumilivu na kuwa kichwa ngumu kwa kufunika kombe na kuwaachia wanaharamu wapite ilihali yeye akiendelea kuchafuliwa kwa tuhuma ambazo mhusika mkuu ana julikana.

Ukweli wake na uvumilivu wake ndiyo ambao ulimponza ikiwa ni pamoja na siasa za chuki za kimakundi zilizokuwa zikiongozwa na kinara wa makundi mh. Sitta.Kilichokusudiwa ni grant ya uwaziri mkuu,ndo maana alipoamua kuwa kilongola kwa kuwaongoza wenzake nini maana ya utawala bora sakata nalo likaishia pale pale.

Huyu ndiye mmsai aliyepata wakati mgumu sana lakini akiendelea kuitesa serikali ya chama chake kila anapotoa tamko kuhusu hali ya maendeleo na mtikisiko wa uchumi kwa taifa dhaifu la Watanzania.

Tunataka ile dhana ya kuvuana gamba na tuhuma mbali mbali ambazo zinazo husu rushwa zianikwe hadharani kuliko kuendelea kumchafua mh. huyu ambaye alikubali kukibeba chama na serikali yake bila kujali aibu bandia aliyosimikwa na chama chake.

Alikwisha sema hakuna alilofanya ambalo JK Hajui,kwa tamko hilo ina maana ameonyesha njia wapi pa kuanzia na kuifanya assignment kwa Mangula kusimamia na kukinusuru chama kwa kutenda haki bila uoga.
 
Rweye

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Messages
16,285
Points
2,000
Rweye

Rweye

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2011
16,285 2,000
Ilimradi watoto wale,una dola ngapi kwa kuandika hvi mkuu? ..poleni wewe,mhisani wako na chichiemu yenu,kazi mnayo.
 
U

UMUCHAMICHI

Member
Joined
Oct 20, 2012
Messages
41
Points
0
U

UMUCHAMICHI

Member
Joined Oct 20, 2012
41 0
kwa maoni yangu mh.lowasa anafaa sana kuwa raisi wetu 2015 kwa sababu kwa kuwa yeye tayari ni tajiri sana ( bila kuhoji huo utajiri kaupataje)hatakuwa na haja tena ya kuiba? atakacho kifanya ni kutafuta sifa so atafanya mambo mazuri tu na mengi sana .au nyie wana jamvi mnaonaje tuwe na raisi maskini?
 
Makala Jr

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Messages
3,396
Points
1,195
Makala Jr

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2011
3,396 1,195
CCM lazima isambaratike ili Watanzania wapate nafuu,Lowassa,JK,Rostam,Chenge,Kinana,Mkapa wamesemwa sana kuhusu rushwa na hata ukiwatazama usoni kama una moyo wa uzalendo basi utasema siyo Lowassa wala JK,ila ni ccm kwanza ife ili wajipange upya lasivyo tutamuenzi sana Mwl.Nyerere bila kutekeleza aliyoyapigania.
 
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,836
Points
2,000
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,836 2,000
Hizi ndio aina za Unknown Flying News.....zinafanana na zile UFO za akina Chagonja na Kamuhanda
 
A

afwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Messages
4,086
Points
1,250
A

afwe

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2010
4,086 1,250
Pole sana! Unajitahidi kufufua wafu!
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
13,991
Points
2,000
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2012
13,991 2,000
kwa maoni yangu mh.lowasa anafaa sana kuwa raisi wetu 2015 kwa sababu kwa kuwa yeye tayari ni tajiri sana ( bila kuhoji huo utajiri kaupataje)hatakuwa na haja tena ya kuiba? atakacho kifanya ni kutafuta sifa so atafanya mambo mazuri tu na mengi sana .au nyie wana jamvi mnaonaje tuwe na raisi maskini?

NIMESOMA COMMENT HII MWILI WANGU WOTE UNAVIBRATE KWA HASIRA NA MACHOZI YANANITOKA

:frusty::frusty::frusty:
 
sammosses

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
1,344
Points
1,500
sammosses

sammosses

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
1,344 1,500
Hizi ndio aina za Unknown Flying News.....zinafanana na zile UFO za akina Chagonja na Kamuhanda
Mnyonge anyongwe lakini haki zake apewe,tumeona uthubutu wake kwa mambo mbali mbali mfano alianzisha shule za kata lakini dhamira yake haikuwa na mwisho huu ambao CCM wameshindwa kuuendeleza strategically japo lengo hasa alilokuwa nalo elimu zaidi kwa vijana,wakishaelimika wanaweza kujiajiri lakini alitaka elimu iwe bora nasi bora elimu,alivaa viatu vyake amebaki kama sanamu hajui aanzie wapi
 

Forum statistics

Threads 1,295,995
Members 498,495
Posts 31,230,159
Top