Kwa kuwa sitarajii kucheat...
Hiyo scenario hainihusu...
Ila kuna rafiki yangu wa kihindi yalimkuta..alikuwa hajui kama mkewe ni girlfriend wa rafiki yake..ingawa mke wa rafiki yake huyo alikuwa anaujua mchezo mzima..
Kuna siku waliamua kwenda disko..kila mtu aje na mkewe.. Wakaanza kufakamia pombe..wakawa wanatoka wanaenda kudensi,ambapo ilikuwa kitu udhungu hivi.. Umamnyanyua shemeji yako time yoyote mziki unaokonga moyo wako unapopigwa...
Ilifikia wakati yule rafiki yangu akawa hamwoni mkewe wala rafiki yake.. Ila shemeji yake alikuwepo,na alionekana kama kakolea kilevi hivi.. Rafiki yangu alipouliza walipo wenza wao,yule mwanamke akasema anajua waliko,hivyo wachukue taxi wawafuate..
Cha ajabu rafiki yangu alishangaa safari ikiishia hotelini,na ni baada ya kuwa ameliwa denda na vituko vingine kadhaa..jamaa akalipa wakaingia room.. Pamoja na malavidavi yaliyoendelea,alishangaa kumwona shemeji yake alivyokuwa relaxed as if hakuna jipya wala la ajabu linaloendelea.
Asubuhi yake rafiki yangu baada ya kubrain storm saaana uongo atakaoutumia kumpeleka shemeji yake kwa mumewe,na kwamba angemuomba rafiki yake waende pamoja kwa mkewe akamsaidie kuapologize..
Cha ajabu pea zote mbili zilikutana lounge! Rafiki yangu alipigwa sana na butwaa.. Alishindwa kuamini kama mkewe ingetokea hata siku moja angemsaliti..ndipo alipoamini maneno ya shemeji yake..kwamba relationship ya mkewe na rafiki yake ilikuwepo muda mrefu!
Alichoniambia yeye hakukasirika,zaidi ya mkewe kuwa katika hali ya kutamani ardhi ipasuke adumbukie ndani. Rafiki yake sasa alikasirika sana,na kumzoa mkewe hobelahobela hadi car park kutafuta taxi bila kuagana na wenzao!
Hiyo ni Dar,na ni kama miaka 15 hadi 20 iliyopita kisa hiki kilipotokea!