KIDUNDULIMA
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 966
- 541
Umehamia katika nyumba ambayo LUKU ya umeme imechezewa. Pia katika nyumba hiyo kuna wapangaji wengine wawili ambao mnatumia kwa pajomaja hiyo Luku. Na kwa utaratibu waliouweka ukakuta kuwa wanachangishana sh. 10,000 kwa kila mpangaji ili kununua umeme. Na umeme ukinunuliwa unaishia tar. 17 ya mwezi na kwa siku zilizo baki LUKU inasoma 00.00 kuonyesha kuwa umeme umekwisha lakini kwa vile imechezewa inaendelea tu kupitisha umeme.
Kutokana na matumizi yenu makubwa ya umeme unajikuta kuwa unafaidika sana na hako kautaratibu kwa vile unachangia hela kidogo kwenye matumizi ya umeme. Baada ya kuishi kwa miezi nane TANESCO wanakuja kuwakamata. Kwa vile wewe sio mmiliki wa ile nyumba unamtaarifu Mwenye nyumba ambaye nae anakuachia mzigo kuwa umalizane na Tanesco maana yeye hana taarifa kuwa LUKU yake imechezewa. Unakwenda kwa vijana wa TANESCO wanakwambia tuongee la sivyo suala liende ofisini ambako wana kutishia kuwa faini ni sh. 5,000,000. Na kigezo wanachotumia kukubana ni kuwa wewe unataarifa kuwa LUKU imechezewa au ni Mbovu na hujatoa taarifa Tanesco. Wana sajest uwapatie sh. 20,000 ili wakurudishie umeme na kwa sharti kwamba umtafute fundi aliyeichezea LUKU airudishe kwenye hali yake ya kawaida.
je utoe sh. 20,000 na urudishiwe umeme au suala lako lipelekwe TANESCo kwa maamuzi mengine?