Ungekua wewe ungefanyaje?

Ungekua wewe ungefanyaje?

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2021
Posts
339
Reaction score
683
Wakuu habarini za leo!?

Lengo kuu la Uzi huu ni kutaka mawazo mbadala ama ushauli kutoka kwenu.

Mm mkazi wa geita mjini mwenye miaka 24, sjaoa na Wala Sina mtoto.

Naweza kusema kwasasa mm ni mzawa wa Geita mjini japo kua skuzaliwa hapa ila nimeishi tangu mwaka 2002 mpaka leo.

Mwaka 2018 mwezi wa 11 nilifungua biashara ya mpesa kwa mtaji wa laki 8 baada ya kua nimelipia kila kitu.

Baadae nikaongeza huduma za mitandao yote mpaka Sasa.

Changamoto
  • Mwaka 2019 Mwezi wa 3 nilitapeliwa laki 3
  • Mwaka 2020 mwaka haukua mzuri kwangu ki biashara.
Mwezi wa 4 mwizi alitoboa "singboard" kwakua flame yangu kwa nyuma ni guest aliingia kulala kama mteja akapanda juu ya uwaz ulio kua chooni na kukwea chuu ya dari la nyuma tukaibiwa flame zote.

Mimi niliibiwa hela cash 1.5 milion + sim viswaswadu nilivo kua naviuza 15 pic.

- Mwezi wa kumi niliamua kuboresha ofisi nikasuka grill kwa juu na nje, kuna siku alikuja mdogo wangu nikamuacha kama dk 20 akaja jamaa kununua sm kumbe alikua tapeli akapigwa sm kubwa infinix smart 5 kwa wakati huo nilipoteza 200k

- Baada ya wiki mbili mbele nikiwa nimefunga kikufuri changu nimeenda kununua vocha upande wa pili mida ya saa 10 jion akaja kibaka akiwa na master key, akafungua kakomeo na kupora simu kubwa smart phones 5 na cash laki 9 = 2.4 milion ya kilicho porwa, ila mungu mwema jirani yangu alimuona mwizi na kupambana nae, nilipo Rudi ofisini nikapigiwa sm mpaka mwizi alipo nikaokoa kila kitu kilicho kua kimeporwa.

- Baada ya wiki mbili nikatuma pesa ki makosa laki 6 na mteja alikua anadaiwa songesha 1000 ilipo katwa nikawa Sina uwezo wa kurejesha muhamala huo hata nilipo piga sm Vodacom sikusaidiwa kwaio nikawa nimepoteza laki 6.

- Biashara ya mazoea ya urafiki. Hii hitokana na baadhi ya marafiki wakikwama hunitimbia nilipo na kuja kunieleza shida zao nakosa namna naamua kuoa Kidogo nawapa.

- Zingine nakumbuka ni changamoto binafsi sio za ofisi, ni zile za matumizi muhimu.

Mafanikio:
Kwa mpesa zamani camisheni ilikua ina Soma 400k kwa voda

Tigo: 60k

Ila kwa Sasa biashara imekua ngumu Sana hivyo naishia kupata 300k

Nilibahatika kukuza mtaji mpaka milion 4.8 mpaka kufikia mwaka 2020 mwezi wa 9. Nikafanya maboresho ya ofisi Kidogo nikaanza kuuza sm kubwa ila kwa ma ingira niliyopo biashara haiwend kabisa. Sm ndogo nauza 1 pic au 2 pic kwa wiki nzima na faida yangu ni 3000 kwa kila pic ya sm. Kwaio nimesitisha biashara ya sm, nimebakiza mpesa.

Location ya biashara:

Nipo geita mjini mtaa wa shilabela. Huu mtaa kwa juu kama 1 km kuna poli lenye vichaka ambapo ni chimbo la wavuta bangi karibu wote wa hapa mtaani na mitaa jirani.

Baada ya kuvuta huja kujichanganya mtaani hivyo mtaa wangu una vibaka wengi sana.

Kwa kua geita haija kaa ki biashara sion mtaa mwingine wa kwenda kufanya biashara, isipokua mtaa wa nyankumbu umechangamka lakin ni nyumbani kwa baba na mama hivyo sihitaji kufanyia huko biashara maana nilijaribu nikaferi.

Maoni yangu:

Ninawaza kuhama mkoa niingie kwenye mikoa ya kibiashara.

Haya mdau nambie ungekua ni wewe ungefanyaje?
 
Hapo mkuu kwenye kazi zinazohusu miamala ya hela ni ngumu kidogo kuwa na ushauri isipokuwa unaweza mwenyewe kufanya research na kuangalia ni mkoa upi Ila unaweza kwenda Katavi pia sio mbaya
 
Sawa kaka Asante, challenge tu hainifanyi kukimbia hapa nilipo, kinacho nifanya nikimbie hapa ni mzunguko wa fedha kwasasa umepungua pakubwa ukiangalia geita wanategemea waajiliwa pekee kufanya mizunguko ya kifedha.

Inshort huu mji haujakaa kibiashara hapa wateja wangu ni wale wanao tokea majumbani na hawa sometimes ni wazuri kwakua wengi wanakua wateja wa kudumu lakin sometimes wanaferisha maana siku akikwama anakuja kukukopa.
 
Fanya biashara huko huko kwasababu challenges zake umeshazijua.

Hata huko unakotaka kwenda changamoto zipo kibao.
Hamia Dar es Slaam
Nawaza hivyo maana mwezi wa 4 nilikuja kufanya research nikaona kwangu mie Ni rahisi kufanikiwa dar kuliko hapa nilipo sema changamoto ni gharama ya maisha Kodi ni kubwa kuliko hapa nilipo.
 
baada ya wiki mbili nikatuma pesa ki makosa laki 6 na mteja alikua anadaiwa songesha 1000 ilipo katwa nikawa Sina uwezo wa kurejesha muhamala huo hata nilipo piga sm Vodacom sikusaidiwa kwaio nikawa nimepoteza laki 6.
Hapo ☝️sijaelewa songesha anaiwa elfu 1 na ww ulituma 600k? Yani ni mteja huyo au mwingine?
 
Ww ni moja kati wapambanaji wasio choka, hongera sana ila:

Kabla hujafanya uamuzi wa kuhama fanya utafiti kwanza wa eno husika,unaweza kuhama jumla mkuu na msingi wote ukafia kwenye matumizi kabla ya kuanza biashara.

Jambo lingine usikariri biashara jaribu pia kila eneo utakalopata angalia linaendana na biashara gani? Hiyo ya miamala inakaa popote haichagui kuwe na watu wengi tu.

Kwa upande wa Dar m-pesa isitegemee kupata kamisheni nyingi kwenye voda, labda tigo na Airtel,voda inakimbiza sana mikoani.
 
Hapo sijaelewa songesha anaiwa elfu 1 na ww ulituma 600k? Yani ni mteja huyo au mwingine?
Hapa mkuu nilikosea namba nikatuma laki6 kimakosa na nilie mtumia alikua anadaiwa songesha elfu moja hivyo sikufanikiwa kurudisha pesa maana niliambiwa mteja kasha itumia kias flan Cha pesa, na ili muamala urudi wote mpaka kiasi kiwemo chote, kikipungua hata sh 100 huwezi rudisha pesa
 
Hapa mkuu nilikosea namba nikatuma laki6 kimakosa na nilie mtumia alikua anadaiwa songesha elfu moja hivyo sikufanikiwa kurudisha pesa maana niliambiwa mteja kasha itumia kias flan Cha pesa, na ili muamala urudi wote mpaka kiasi kiwemo chote, kikipungua hata sh 100 huwezi rudisha pesa
Ungewaambia warudishe hicho hicho wangekubali au kuzuia mkuu, dah!!🤔 Mimi niwah kukosea wakarudisha
 
Ungewaambia warudishe hicho hicho wangekubali au kuzuia mkuu, dah!! Mimi niwah kukosea wakarudisha
Ilikua mwaka gani mkuu? Maana Mimi niliwaomba wakakataa wakasema niende police. Afu sjui inategemeana na mtoa huduma kuna wengine hawana huruma yan wanakujibu majibu ambayo yanaonesha kua hataki usumbufu, ila wengine huonesha nia ya kukusaidia kabisa.
 
Ilikua mwaka gani mkuu? Maana Mimi niliwaomba wakakataa wakasema niende police. Afu sjui inategemeana na mtoa huduma kuna wengine hawana huruma yan wanakujibu majibu ambayo yanaonesha kua hataki usumbufu, ila wengine huonesha nia ya kukusaidia kabisa.
Hii mitandao ukiongea nao kwa upole hawawezi kukusaidia. Koroma nao tena waambie mm naenda TCRA mana wana haki ya kukusaidia mpaka pale watakaposhindwa
 
Hii mitandao ukiongea nao kwa upole hawawezi kukusaidia. Koroma nao tena waambie mm naenda TCRA mana wana haki ya kukusaidia mpaka pale watakaposhindwa
Dah kama sasaiv wanauliza kwanza sehem uliyopo Sasa sjui ndo Wana angalia(ga) na maeneo wakijua huwez kufanya chochote.

Mafano juzi kati hapa kuna jamaa yangu ilikuja kutuma pesa laki moja kwa bahati mbaya akakosea namba moja afu hakuniandikia jina kwenye kile ki karatasi mm nikatuma hela, baadae akarud akadai Alie kua anamtumia hajaiona pesa kuangalia namba akakuta kakosea.

Sasa kwenye kurudisha mm nikashindwa ikabidi nipige sm kuwaomba kurudisha, akapokea kaka mmoja iv asee huyo bro ni mpuuzi Sana, huwez amini aligoma kurudisha muamala anasema eti nirudi nikajihudumie maana mteja bado hajaitoa hiyo pesa.

Baadae tukabishana akanitema, nikarudia kuzuia muamala sikufanikiwa. Nikapga sm tena akapokea mdada huyo ndo akanisaidia kusitisha muamala asee nilitafakari Sana hii kazi.

Usalama wa pesa kwa wakala kwa Sasa haupo kabisa yan wakala akikosea kutuma pesa hapati msaada wowote wakati kwanza campuni linamtumia yeye kujibrand na kutatua shida zile ndogo ndogo za wateja wa voda.

Hii biashara sometime inachosha akili bro. Dah
 
Back
Top Bottom