mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,072
Uwajibikaji ni dhana yenye sifa,heshima na tunu kwa anaewajibika kiutendaji katika majukumu ya kimamlaka au dhamana kiuongozi kisiasa,kijamii na n.k. Ung'ang'anizi katika madaraka ni dhana yenye mwerekeo wa kuficha udhaifu,uchafu,uozo na ufisadi.Mara nyingi mwenye kustahili kuwajibika asipowajibika huwajibishwa kwa hiari au mgandamizo au msukumo toka ndani au nje.
Kwa yanayoendelea nchini kwetu japo twaweza fumba macho na masikio yetu kana kwamba hatuoni wala kusikia yanayojiri lakini ukweli utabaki kuwa ukweli na uongo kuwa uongo...Kuna mambo yanaumiza sana jamani,ni mateso ni shida kubwa kwa wasio na sauti/wasiosikika/wasio na kimbilio...Inasikitisha sana ya kuwa tumefikia hatua ambayo matajiri wamekuwa adui wa maendeleo badala ya chachu ya maendeleo kupitia kodi wanazolipa,ajira watoazo kwa maskini.Nchi yetu inapaswa kupiga hatua kubwa kimaendeleo kupitia viongozi wenye kumcha Mungu katika roho,nafsi na kweli..Baadhi ya viongozi wanamdharau Mungu na uweza wake kwa kutumia madhabahu kama blanketi la kufunika uozo wao,unyama wao,chuki zao,visasi vyao...
Viongozi watenda haki na wasimamia haki,sio viongozi wabinafsi,wenye viburi,wenye kiu za utajiri,husuda,faraka,tamaa mbaya,wenye kutumia majina ya viongozi waadirifu kujinufaisha,wenye kutesa wananchi,wenye kunyanyasa wananchi,wasiojua dhana ya uwajibikaji...
Enough is enough...Its high time justice should prevail in our beloved country...