Undugu kati ya uchawi na soka

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,736
155,419
attachment.php

MASHADANKA YAKIWA KATIKA GLOVS ZA KIPA WA TOTO ALIYOKUWA AMEHIFADHI GOLINI MWAKE HATIMAYE YALIFUKUNYULIWA NA MNAZI MOJA WA SIMBA (ANAYEYAANIKA KWA WANDISHI WA HABARI), DAKIKA CHACHE BAADAYE SIMBA WALIOKUWA HAWAONANI WAKAANZA KUONANA, MUSSA HASSAN MGOSI AKAFUNGA GOLI LA KWANZA NABADAE RAMADHANI CHOMBO 'REDONDO AKAONGEZA JINGINE WAKATI SIMBA ILIPOPATA USHINDI WAKE WA 14 MFULULIZO BAADA YA KUIFUNGA TOTO 2-0.
attachment.php

SHABIKI HUYO ALIYEWAUMBUA TOTO ILE KIPUTE KINAMALIZIKA TU NA REFA KUPULIZA KIPYENGA KUASHIRIA NGOMA METII ALIANGUKA UWANJANI HAPO NA KUANZA KUPEPEWA. SAMBAMBA NA HILI VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO WACHEZAJI VILIKUTWA VIKIWA VIMETAPAKAA DAMU ISIYOJULIKANA NI YA MNYAMA GANI.
 

Attachments

  • KIPA1.jpg
    KIPA1.jpg
    19.9 KB · Views: 158
  • image002.jpg
    image002.jpg
    23.8 KB · Views: 156
Nilishawahi beba hirizi wakati nacheza soka, miaka ya tisini . wakuu kitu kinapumua kweli usifanye masikhara, Tulichoambiwa cha kutisha, kwanza hakuna kufanya mapenzi 24hrs before match, halafu lazima uoge kabla ya kwenda kwenye mechi, halafu ukiwa uwanjani ukabana na mpinzani wako km ana hirizi basi zitashindana itakayoshindwa yule aliyebeba anaweza vunjika mguu au kiungo chochote kile, kingine mkimwona mtu aliyebeba hirizi amedondoka chini from nowhere kimbieni toeni hirizi ikojoleeni itaisha nguvu, lkn mki mkimbiza hospitali bila kutoa hirizi akichomwa sindano tu basi ndo safari hiyo kwishnei no LIFE.Ndo yaliyowatokea akina Sembuli uwanjani haya. Soka letu haliwezi kukua hata siku moja bado miushirikina ipo mno kwenye mind za viongozi wa timu zetu
 
nilishawahi beba hirizi wakati nacheza soka, miaka ya tisini . Wakuu kitu kinapumua kweli usifanye masikhara, tulichoambiwa cha kutisha, kwanza hakuna kufanya mapenzi 24hrs before match, halafu lazima uoge kabla ya kwenda kwenye mechi, halafu ukiwa uwanjani ukabana na mpinzani wako km ana hirizi basi zitashindana itakayoshindwa yule aliyebeba anaweza vunjika mguu au kiungo chochote kile, kingine mkimwona mtu aliyebeba hirizi amedondoka chini from nowhere kimbieni toeni hirizi ikojoleeni itaisha nguvu, lkn mki mkimbiza hospitali bila kutoa hirizi akichomwa sindano tu basi ndo safari hiyo kwishnei no life.ndo yaliyowatokea akina sembuli uwanjani haya. Soka letu haliwezi kukua hata siku moja bado miushirikina ipo mno kwenye mind za viongozi wa timu zetu


mjomba wangu alianguka uwanjani ghafla,
na kweli walimkuta na hirizi,
alipochomwa sindano ndio ukawa mwisho wa maisha yake.
Mungu ailaze roho yake mahali pema.
 
Afrika moto, Afrika nyumbani.......ndo raha ya soka la nyumbani Tanzania .
siasa ina Uchawi, elimu kwa uchawi, utajiri uchawi, soka uchawi, mapenzi uchawi, ndivyo tulivyo.
 
sio Tanzania tu, imani ya uchawi na soka ni almost Africa nzima
 
iwe unasaidia ama hausaidii, lakini soka la Afrika nimetawaliwa na kila IMANI za ushirikina, ndumba ama Uchawi.
sasa miaka kumi nyuma , unaambiwa watu walikua wanakwenda mochwari pale muhimbili kuiba maji ya kuoshea maiti, kwa ajili ya kazi hiyo. ipo simulizi pia haya maiti zilikua zinaibwa kwaajili ya kwenda kufanikisha mambo hayo, hasa mechi ya Simba na Yanga.
kumbuka kisa cha kipa aliekua anaitwa Mchopa, aliuawa kiajabu kule sokoine Mbeya, hadi leo si wachezaji wenzake, si daktari wa Timu alieweza kutoa majibu hasa ya nini kilimchinja kipa yule.
Nzoysaba aliwahi kunukuliwa akisema , kijana alichinjwa na kisu kisichoonekana. Afrika moto.
 
Back
Top Bottom