Under this situation nothing shall be achieved

optimist

JF-Expert Member
Sep 13, 2009
281
98
Ilikuwa tarehe 10 june 2013 siku ambayo walimu wa masomo ya sayansi mkoani lindi walipokutana lindi sec kwa ajili ya kuwajengea uwezo wao katka umahili wa kufundisha masomo yao lakn cha kushangaza walimu walivotoka mashuleni kwao waliambiwa stahiki zao watalipwa na waandaaji wa semina hiyo ambao ni Moevt na wadau wengine, chakusikitisha walimu hao walilipwa elfu 15 kwa siku ikiwa ni pesa ya kujikimu huku wengine wakalazimika kulala mabwenini baada ya kushndwa kumudu ghrama za malazi aidha katka kujadili na kutafuta ufumbuzi baada ya walimu kutoridhika na hoja za uongoz wa elimu mkoa ikabidi wawe msimamo wa kuahirisha semina mpaka watakapohakikisha kuwa maandaliz yamefana, mwenye kiti wa tahosa mkoa akaropoka kuwa hatuna muda wa kubembeleza hvyo aliye tayar na semina aendelea asiyetaka asepe mlango uko waz , mkasa mzma unaskitisha na kada ya elimu huu ni udharirishaji.
 
Hayo mambo siyo Mtwara tu, Mwaka jana semina kama hizo zilifanyika katika Mkoa wa Mwanza Walimu walisafiri kutoka KWIMBA,SENGEREMA,MAGU,MISUNGWI,ILEMELA, NYAMAGANA mpaka UKEREWE ndiko kulikofanyikia hiyo semina kilichotokea huko ni kwa walimu kunyimwa posho zao na wakaambiwa kuwa fedha watalipwa na wakuu washule, Na walimu walipo goma wakapewa vitisho hivyo hivyo na hata wale walioamua kuondoka waliondolewa katika orodha ya kusimamia mitihani yote ya kitaifa na amri hiyo ilitokana na makubaliano kati ya maafisa elimu na vibaraka wao TAHOSSA. Katika vyama vya kitaaluma vinavyopaswa kufutwa hapa nchini kikiwemo TAHOSSA ni wakandamizaji sana wa WALIMU na ukifanikiwa kuhudhuria vikao vyao kazi yao kulishana uongo na kuongelea namna ya kudhibiti walimu siyo kuboresha elimu. Ndio hao wanaoeneza uongo kuwa walimu wanaotoka vyuoni hususani wenye shahada kuwa ni wakorofi na hawana maadili,lakini ukiwachunguza wao ndio walafi wakubwa wa fedha za CAPITATION, na ndio maana shule nyingi hazina vifaa ukijiuliza fedha zinazoyolewa na serikali na michango ya wanayokusanya kutoka kwa wanafunzi zinafanya kazi gani?
 
Back
Top Bottom