Unconditional Love

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,936
3,958
Mwanaume na msichana mmoja walikuwa katika mahusiano. Baada ya miaka kadhaa ya mahusiano yao, mwanaume alimaliza chuo kikuu na kuamua kujiongezea maarifa kwa kwenda kusoma nje ya nchi.

Kabla ya kuondoka nchini, alitoa mapendekezo ya uchumba kwa yule binti. "Yule kijana alimwambia binti, mimi sio muongeaji, ila ninachojua ninakupenda sana, kama utaniruhusu kukuoa, nitakua mwanaume wa maisha yako yote.

Msichana alikubaliana nae na wakaenda kutambulishana kwa wazazi.

Wazazi wa pande zote walikubaliana vijana wao waoane kwani ni kweli walionesha kupendana sana. Ila kabla ya kuondoka kijana alimvisha pete ya uchumba na kuahidi kufunga ndoa pindi atakaporudi nchini.

Binti aliendelea na kazi yake huku kijana nae akipaa kwenda ng'ambo kujiendeleza kielimu. Walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara kupitia emails na kupigiana simu.

Ingawa mapenzi ya mbali yalikuwa magumu kwao, ila kamwe hakuna aliyeonesha kukata tamaa.

Siku moja wakati msichana akielekea kazini, aligongwa na gari lililokua limepoteza mwelekeo. Alipoteza fahamu palepale na siku alipoamka aliwakuta wazazi wake wakiwa karibu yake. Akatambua kwamba yupo hospitali na ameumia vibaya.

Alipomwona mama yake akilia, akataka aongee kitu lakini akagundua hakuna sauti iliyokua inatoka..alipoteza sauti yake. Daktari akatoa ripoti kuwa ubongo umepata madhara na hvyo kupoteza uwezo wa kuongea. Pia mguu wake wa kushoto ulivunjika na kushindikana kuunga tena.

Baada ya kutoka hospitali, binti aliendelea kuuguzwa huku mchumba wake akipiga simu kila siku. Binti hakupokea wala hakutaka mtu yeyote amwambie yule kijana hali yake. Hakutaka awe mzigo kwa yule kijana.

Hivyo alimwandikia barua na kumwambia kua ameshindwa kusubiri hvyo aendelee na maisha yake. Katika barua aliambatanisha na ile pete ya uchumba aliyovishwa kabla yule kijana hajaondoka.

Baada ya kupata ile barua Kijana alijitahidi kutuma barua na kupiga simu mara kwa mara kumbembeleza lakini binti alikuwa akilia tu na kutojibu lolote.

Wazazi wa binti wakaamua kumhamishia mbali wakitaraji kwamba atasahau kila kitu na kuwa na furaha tena.

Katika mazingira mapya, binti alijifunza kuongea kwa vitendo (sign language). Huku akijiambia nafsini mwake atamsahau yule kijana.

Siku moja rafiki yake alimtembelea na kumweleza kuwa yule kijana amerudi nchini. Yule binti alimwomba sana rafiki yake asimwambie yule kijana kwamba yupo pale na asimweleze chochote kuhusiana na yaliyomtokea.

Baada ya hapo hakukua na taarifa tena juu ya yule kijana.

Mwaka mmoja ukapita, na siku moja yule rafiki yake akaja kwa yule binti na kumpa bahasha iliyokua na kadi ya mwaliko wa harusi ya yule kijana. Yule binti aliumia sana moyoni mwake.

Lakini baada ya kufungua bahasha, aliona jina lake kwenye ile kadi. Alipotaka tu kumuuliza yule rafiki yake kwa saini za vitendo, alimuona kijana akiingia ndani.

Yule kijana akatumia lugha ya vitendo na kumwambia "Nimetumia mwaka mzima kujifunza lugha ya vitendo ili niweze kuwasiliana na wewe na kukueleza kwamba, ingawa umepatwa na matatizo makubwa, bado sijasahau ahadi yangu kwako. Nipe nafasi mimi niwe sauti yako. Nakupenda sana..."

Yule binti na Kijana walioana, Mungu amewabariki na watoto watatu, wanaishi kwa upendo huku vicheko na tabasamu ukiwa wimbo wa taifa wa ndoa yao.

Ni wazi kuwa pale unapofikiri umepoteza matumaini kabisa, ndipo kipindi ambapo msaidizi wako atakapotokea. Haijalishi tatizo gani mwenzio anakumbana nalo, kamwe usimuache peke yake. Kuweni kama timu yenye kiu ya mafanikio.

Kuwa sauti yake pale anapopoteza sauti, kuwa mwanga wake pale anapopoteza matumaini na panapo mafanikio basi furahini pamoja.

Mwenyezi Mungu akubariki wewe uliyesoma ujumbe huu, akujalie mtu ambae utakua nae bega kwa bega katika hatua za kimaisha na kamwe asikuache..!!

AMEN!
 
amezing
 
Inafurahisha sana...
Hayo ni mapenzi na uvumilivu wa mwanaume kwa mwanamke...

Je?

Mwanaume angepatwa na hayo maswahiba... Mwanamke angemvumilia?

Cc: mahondaw
 
Aya mapenzi ya apa bongo!?,ukiniambia ndio i will die laughing bwahaaaaaaaaa,Aaaa wapi nyie endeleeni nayo,..sie tupoo mapenzi yetu ni pesa,..better look something worth to do,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom