Unawezaje kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni au taasisi

Shepherd

JF-Expert Member
Dec 14, 2012
2,425
1,653
Jambo hili linawezekana kwa namna nyingi.

Hila kwa hapa nazungumzia umiliki wa kampuni kupitia hisa. Hisa ni kitu cha kiusalama na kihalali kinacho mwezesha mtu kuwa na umiliki wa kampuni au tahasisi husika. Mwanahisa ni mtu ambaye anaumiliki wa kuanzia hisa moja na kuendelea,kwa dhana hiyo ukiwa na hata hisa moja tayari wewe ni mmiliki wa kampuni au tahasisi,pia una haki ya kujua kila kinachoendelea kwenye kampuni,pamoja na kufaidi faida au hasara inayopatikana ukiwa mwanahisa.

Hivyo basi unaweza kuwa mmiliki wa kampuni kupitia hisa.
 
Hisa ni nini tafadhali? Na ni namna gani naweza kununua hizo hisa na ninazinunua wapi?

Fikiria Kwa Mfano Tunaanzisha Kampuni Watu Watatu, Mtaji wa Kampuni ni Shilingi Milioni Moja. Bwana A Anachangia Laki Tano ya Mtaji Sawa na 50%, Bwana B Anachangia Laki Mbili na Nusu Sawa na 25 na Bwana C Anachangia Laki Mbili na Nusu Sawa na 25%.

Sasa, Ili Kila Mtu Apate Mgawanyo Sawa wa Faida Unaoendana Kiasi Alichochangia.. Ndio Kila Mtu Anakua na Document Maalum Inayoonyesha Kiasi cha Umiliki Wake Kwenye Kampuni, Document Hiyo Huitwa HISA.

Ina Maana, Kampuni Ikifanya Biashara na Ikipata Faida ya Milioni Mbili, Bwana A Anayemiliki 50 ya Hisa Atapata Gawio la Shilingi Milioni Moja, BwanaB na Bwana C Wote Wanamiliki Hisa za 25% Kila Mmoja Atapata Laki Tano.

Gawio Ndio Huitwa Dividend.

Sasa Hizo Hisa Katika Hatua ya Kwanza Huitwa Primary Market. Kampuni Ikiingia Kwenye Soko la Hisa (Dar es Salaam Stock Exchange Market -DSE) Wale Wanahisa wa Mwanzo Wana Uwezo wa Kuuza Hisa Zao. Mfano Bwana A Anaweza Kuamua Kuuza Asilimia 25 za Hisa Anazomiliki Kwenye Kampuni. Na Hata Wewe Unaweza Kwenda Kununua Vipande na Ukawa Sehemu ya Wamiliki au Wanahisa wa Kampuni Japo Hukushiriki Kipindi cha Kuanzisha Kampuni. Inategemea na Bei Husika Lakini Kipande Chaweza Kuanzia Shiligi Mia Tatu au Vinginevyo.Hiyo Ndio Inakua Secondary Market.Gawio Hufanyika Mwakani na Bila Shaka Ushawahi Kusoma Matangazo ya Mkutano wa Wanahisa wa Kampuni Fulani.

Hope Utapata Picha Mkuu, Nimejaribu Kurahisisha Sana Kwa Ajili ya Uelewa. Wataalam Watakufafanulia Zaidi.
 
Hongera sana Bw.Dafa umeweka nyama za kutosha hata mimi na weza miliki Newcastle endapo tu nitanunua hisa zake.
 
Back
Top Bottom