Unaweza kuwa mzalendo kwa taifa lako kupitia vyama vya siasa?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Ukiwaangalia makada wa chama tawala wanajiona wao ni wazalendo wa taifa hili kuliko mtu yeyote yule na wamejipa hakimiliki ya taifa kwa kila kitu, ikitokea uwe upande wa upinzani unaonekana wewe sio mtanzania na mhalifu kabisa....

Pia kwenye vyama vya upinzani kumejengwa mtazamo huo kuwa wao ni bora zaidi mbele yauso wa Taifa, na kwamba wale wa Chama tawala ni wahalifu na wasaliti kwa taifa hili.

Hii ndio mitazamo ya watu wote katika siasa, na kwa bahati mbaya kila kitu nchini kinaendeshwa kisiasa.

Hebu fuatana nami tujifunze mambo machache juu ya haya...

Kwanza tujiulize, Siasa ni nini?

Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni njia azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia. Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani.

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa yake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa. Mpaka hapo tumeshafahamu mwanasiasa ni mtu wa aina gani katika taifa,

Je Itikadi ni nini?

Itikadi ni mkusanyiko wa imani unaoshirikiwa na kikundi cha watu fulani. Kuna aina kuu mbili za itikadi: Itikadi za kisiasa, na itikadi za kiepistemolojia (ni sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo). Itikadi ya kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na vipi nchi itaendeshwa. Itikadi za kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu wanapaswa kufanya maamuzi. Kwakuwa dhamira yetu ipo kwenye mkondo wa siasa, hivyo tujikite kuangazia itikadi ya kisiasa zaidi katika mukthada huu.

Ulishawahi kujiuliza kwanini vyama vya siasa Marekani, Israel, Italia, Urusi nk, havitumii bendera wala nembo zao ktk mikutano ya hadhara?

Na sio kwamba havina nembo na bendera, bali havizitumii kama ilivyo kwa siasa za Afrika.

Kwa taarifa yako wenzetu ili kulinda uzalendo wa watu kwa taifa lao, huendesha siasa kwakuzingatia viashiria vya ukuu wa uzalendo na utaifa.......Hili kwa Tanzania Mwalimu Nyerere alikosea sana pale alipotilia mkazo kujenga kunguvu ya chama badala ya kujenga nguvu ya misingi ya utaifa wetu, badala ya kujenga nidhamu ya taifa, yeye akajenga nidhamu ya chama kilichoshika hatamu, Yaani chama kilikuwa na nguvu kuliko serikali na taifa... Hali inayopelekea kuwa chama kikianguka na taifa linaanguka.

Mwanafalsafa Plato anasema, "Serikali ya kidemokrasia ya watu wapumbavu ni hatari zaidi kuliko serikali ya kidikteta ya watu wapumbavu"...

Nawaomba someni vitabu na nyaraka hizi hapa chini kwa faida yenu marafiki zangu...

National identity
National identity - Wikipedia, the free encyclopedia

Do we need nationalism today? Why?
Do we need nationalism today? Why? | POST

What Is The Meaning And Importance Of Nationalism Politics Essay
What Is The Meaning And Importance Of Nationalism Politics Essay

Nationalism in the 21st Century
Nationalism in the 21st Century

The New Age of Nationalism
The New Age of Nationalism
 
ulianza vizuri mwishoni ukajichanganya kuwa mzalendo hakuhitaji kuwa mwanasiasa tumeona wanajeshi wanavyojitoa mhanga kutetea nchizao wakati wa vita wao si wanasiasa ila ni wazalendo sema baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi imejenga dhana ilii ufanye kitu kwa taifa lako inabidi uwe mwanasiasa matokeo yake tumezalisha matapeli wengi wa kisiasa ambao wameweka maslahi yao mbele bila kujali nchi inahitaji nini mfano posho wanazojilipa
 
Kama siasa ni itikadi ya kuendesha uchumi,utamaduni na mwenendo mzima wa jamii.
Basi tunapungukiwa wanaopanga na kuweka hali ya mwelelekeo wa uchimu,utamaduni na mwenendo. Hawa ni wasomi ambao wamemezwa na katiba yao wenyewe iliyotungwa na kuifunga taaluma ya wasomi na lufanya wasomi bendera fuata upepo wa wanasiasa na chama tawala ambacho kimepewa mamlaka kikatiba kutawala karne hadi karne.

Tatizo kubwa lilikuwa kipindi kile tunapokea vyama vingi tulilazimishwa watu wengi hawakukubali huu mfumo.Ndio maana wanazuoni walikipa nguvu ya kikatiba chama tawala ambapo kimsingi na uhalisia utaona kwamba hakuna mfumo wa vyama vingi tanzania.
Bali tunatembea kwenye kivuli cha vyama vingi leo hii tunakuja gundua wakati tumekwisha chelewa sana.
 
Mzalendo ni mwananchi yeyote alie na asiye na chama mwenye kujali utu,haki na kutimiza wajibu wake
kwa mujibu wa katiba ya nchi kwa wakati uliopo na ujao.

Uzalendo ni tunu ya utaifa na upimwa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwa na hofu ya Mungu.
 
Sijawahi kuwaamini wanasiasa tangu nizaliwe.Vyama vya siasa ni vikundi vya kimaslahi vyenye lengo kuu la kushika dola.Lengo kuu ni kutwaa madaraka/utawala ila mbinu za kutafuta 'legitimacy' kwa jamii zinatofautiana baina ya hivyo vyama.Na pia zipo siasa za namna mbili;siasa makini na siasa uchwara.Kwa bahati mbaya sana au kwa makusudi,barani Afrika;hususani Tanzania,siasa uchwara ndio imetawala.Na ndio sababu basi,nchini mwetu tuna 'utajiri Mkubwa' wa wanasiasa uchwara.Angalau huko ng'ambo ipo siasa na wanasiasa makini,lakini haiondoi ile dhana ya 'struggle for power'.
 
Sijawahi kuwaamini wanasiasa tangu nizaliwe.Vyama vya siasa ni vikundi vya kimaslahi vyenye lengo kuu la kushika dola.Lengo kuu ni kutwaa madaraka/utawala ila mbinu za kutafuta 'legitimacy' kwa jamii zinatofautiana baina ya hivyo vyama.Na pia zipo siasa za namna mbili;siasa makini na siasa uchwara.Kwa bahati mbaya sana au kwa makusudi,barani Afrika;hususani Tanzania,siasa uchwara ndio imetawala.Na ndio sababu basi,nchini mwetu tuna 'utajiri Mkubwa' wa wanasiasa uchwara.Angalau huko ng'ambo ipo siasa na wanasiasa makini,lakini haiondoi ile dhana ya 'struggle for power'.
Sio wote mkuu, tumia mda wako vizuri kuchunguza na kuchambua
 
Sina haja ya kusoma thread yako kv tangu zamani msimamo wangu ni kwamba tatizo la msingi kwa nchi kama Tanzania ni vyama vya siasa na wafuasi wao and I don't care kama upo chama tawala au cha upinzani... kwangu mimi wote hao ni majipu kv more often than not; watakuwa mbele kutetea vyama vyao zaidi kuliko kinyume chake!! Kinachosikitisha zaidi ni ile tabia ya wafuasi wa kawaida wanavyofikia kujiona ni kama sehemu ya mfumo wa chama ba/serikali wanayoiunga mkono! Kutokana na ujinga huu ndo pale unakuta wale wale ambao kwa miaka kadhaa wamekuwa wakiwaita baadhi ya watu ni mafisadi wasiofaa kupewa hata uongozi wa mtaa leo hii wamebadilika na kuwaona ndio mashujaa pekee nchi hii wanaoweza kufuta uozo uliopo! Hawa wanafanya hivi kv wanadhani nao ni sehemu ya mfumo na mfumo wao (inner circle) wamewakubali wale wale ambao kwa miaka nenda rudi walionekana reject huku hivi sasa zikitolewa justification mbali mbali za kijinga!!

Ukirudi upande wa pili nako ndo wanaboa unaweza kutamani uwatandike risasi! Utafikiri ni kizazi cha Mfalme Juha, wao wapo kutetea na kuunga mkono kila kinachofanywa au kusemwa na serikali hususani mkuu wa nchi! Yaani Mkuu wa Nchi kwao ni kama Mungu asiyepaswa kuhojiwa kwa lolote!

Namshukuru Mungu nimekataa katakata kuwa mtumwa wa mfumo wa kisiasa!
 
Sio wote mkuu, tumia mda wako vizuri kuchunguza na kuchambua
Mkuu Yericko Nyerere, Lowasa ulimpinga kwa nguvu zote kabla hajaja upande wako, alivyokuja upande wako ulimkubali na kumnadi kwa nguvu zako zote. Je, wewe tukuamini? Na Lowasa vipi?
 
Back
Top Bottom