Unawakumbuka mabingwa wa kugandisha fimbo enzi hizo shuleni kwenu?

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,047
21,522
Salam wakuu,
Swala la fimbo mashuleni (enzi hizo, 1990's - late 1990's) lilikua halina mjadala. Kuna walimu walikua wanajulikana kabisa kwamba ikiingia kwenye kilengeo chake lazima ujute kuzaliwa. Au ufanye msala uitwe ofisini kwa walimu lazima uandae nguvu. Sasa pamoja na wahuni kubuni njia ya kujaradia ili mboko zisiingie fresh lakini kuna walimu ilikua ni kama umejidNganya mwenyewe ngoma lazima uifeel. Still, kuna magwiji walikua ni ma master wakugandisha fimbo aisee. Sisi shuleni kwetu nawakumbuk wafuatao:
1. Munanka Gweso
2. Josiah Kahabi
3. Edgar Filikunjombe
4. Abdallah Jimbi.
Hawa ma mwambA walikua hata apigwe stiki kumi lakini hakuni wala nini anarudi huku anacheka. Tukawa tunawaita manunda. Mimi nlikua naforce kugandisha siku demu nliokua namtokea darasani kama amehudhuria class. Nakaza Ila chozi lazima Kwa mbali. Je, skul kwenu kulikua na miamba gani? Let's share old gold memories...
 
Shamimu Mdoligo
Kimata Saidi
Paskali chusi

Popote mlipo nyie majamaa mlitisha sana kwa kugandisha fimbo. Binafsi nilkua nasingizia ugonjwa na ticha akinichapa tu najiangusha maksudi nafanya kama punda anaekaribia kukata roho ticha lazima apagawe.
 
Hahaha, huyo jamaa shamimu mdoligo anaonekana alikua machafuko sana
Shamimu Mdoligo
Kimata Saidi
Paskali chusi

Popote mlipo nyie majamaa mlitisha sana kwa kugandisha fimbo. Binafsi nilkua nasingizia ugonjwa na ticha akinichapa tu najiangusha maksudi nafanya kama punda anaekaribia kukata roho ticha lazima apagawe.
 
Back
Top Bottom