thewajibu
JF-Expert Member
- Jan 14, 2017
- 226
- 292
Miongo kadhaa iliyopita nilizaliwa huko wilayani chato, tarafa ya nyamirembe katika mojawapo ya kaya kubwa kabisa kijijini kwetu ambapo mgeni aliwaza mara mbili mbili kabla ya kuingia kwenye kaya hiyo kutokana na ukubwa wake na wingi wa watu waliokuwepo.
Ni mengi niliyashughudia yakifanyika na mengine kuyashiriki yaliyohusu waganga wa kienyeji yakilenga ulinzi wa familia, mali na mambo mengine.
Nilichokigundua waganga wanachofanya nikukuunganisha kwenye mnyororo wa thamani na kukuonesha mazingaombwe yenye ukaribu na ukweli ili uwaamini na waendelee kupiga pesa.
Pamoja ulinzi na dawa za wanganga wakutosha lakini familia hiyo kubwa ilisambalatika kabisa huwezi jua kama kulikuwa na kaya mahali pale mpaka mzaliwa wa pale kama mimi
Sitasahau 2002 Mama angu mkubwa alipougua ukimwi miaka hiyo tunaiita (silimu) waganga wengi walikuja na kudai kalogwa na kuondoka na ng'ombe baadae ikagundulika ni mwathilika lakini tayari familia imepata hasara.
Mama mzazi 2008 huenda angepona lakini waganga wa kienyeji walihusika pakubwa katika kifo chake huenda angepelekwa kwenye hospital kubwa angepona kifua pekee kilimsababishia kifo Mungu awaangalie ipasavyo.
Mwisho naandika kwa masikitiko sana ninavyoandika hapa Mama mkubwa mwingine pamoja na dada zangu watatu wameingia kwenye mtego wa maostadhi nimejaribu kuwambia sana lakini hawaelewi mwishoe mimi ndo nikataka kuwa adui wao nimeamua kuachana nao lakini kusema ukweli wanamaliza mali za mama mkubwa.
Sitawaamini waganga hata kama wataumba mbingu mpya na kama ntalazimika nitakufa lakini sitaki waganga wa kienyeji.