Unatakiwa kufikiri kwa kina, usipokee tu unachoambiwa au kuona

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
UNATAKIWA KUFIKIRI KWA KINA USIPOKEE TU UNACHOAMBIWA AU KUONA

Hebu pata picha ungekuwa unaishi mwaka 1950, ambapo hakukuwa na mtandao wa intaneti na hivyo chochote ambacho unataka kujua inahitaji uende maktaba, uanze kupekua vitabu ndio upate.

Lakini hatupo zama hizo tena, sasa hivi tunaishi kwenye dunia ya sekunde sita, kama kuna kitu hujui unaweza kujijua ndani ya sekunde sita tu.

Unachukua simu yako, unaingia google na kuandika kile unachotaka kujua. Tena google ikihisi umekosea itakuletea maelezo ambayo inafikiri ulikuwa unamaanisha.

Kuwepo kwa google kumerahisisha sana mambo na kujifunza kwa sasa kumekuwa rahisi mno, mno. Lakini pia uwepo wa google umekuja na changamoto mpya, ambayo ni watu kuwa na utegemezi mkubwa sana kwenye mitandao ya aina hii.

Watu wanapokutana na changamoto wamekuwa hawafikiri tena, badala yake wanakwenda google na kuuliza swali, majibu yanakuja na wanayachukua na kufanyia kazi. Sasa ingekuwa vizuri sana kama kila kitu kingewezekana hivi, lakini sio vyote vinawezekana.

Kuna maswali ambayo google haiwezi kujibu kabisa, hata ungeuliza mara ngapi, hata ungeuliza kwa lugha gani. Na ni maswali haya ambao ni muhimu sana kwako ili kufanya maamuzi bora kwako na kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Kama unataka kujifunza kupika pilau nenda google na andika, JINSI YA KUPIKA PILAU, na utaletewa maelezo ya kutosha ya jinsi ya kupika pilau. Kama unataka kujua historia au data zozote uliza tu google na utaletewa majibu.

Ila sasa tuseme umepata kazi maeneo mawili tofauti, na yote unaona kama uanakufaa, uchukue kazi ipi na ipi uiache, uliza google mara kumi hutapata jibu.

Au upo kwenye mahusiano ambayo yamekuwa yanakupa changamoto kubwa, unafikiria kuyamaliza mahusiano hayo na usonge mbele, na wakati huo pia unafikiria kuendelea kuwepo kwenye mahusiano hayo.

Google haiwezi kukupa jibu la uhakika hapo.

Maswali yote ambayo yanahusu hali fulani unayopitia wewe kama wewe, google haiwezi kuyajibu, kabisa.

Ni maswali haya ambayo yanakuhitaji wewe ukae chini na ufikiri kisha uje na majibu ambayo yatakufaa wewe kulingana na hali unayopitia.

Yote haya ni kusema kwamba japo teknolojia imerahisisha sana utafutaji wa majibu, bado tunahitaji kutumia akili zetu kufikiri kwa kina kuhusu jibu lolote tunalolitaka au tunalolipata.

Maana kutegemea teknolojia moja kwa moja kwa kila jibu unalotaka, utafika kwenye hali ambapo huwezi kupata majibu zaidi ya kufikiri wewe mwenyewe.

Jenga uwezo wako wa kufikiri kwa kina, utakusaidia kwenye maeneo mengi ya maisha yako.
 
Umenena vema mkuu, niliwahi kuambiwa na Baba mzazi, 'siku hizi hamsomi kwa kutafakari kabisa, hesabu ndogox2 na ramani ya ulimwengu na mabara yake, hamujifunzi kwa ufasaha'. Binafsi sikumbishia, maana kila jambo dogo siku za leo, ni kutafuta tu bando na kujiunga, mbaya zaidi hata walimu (baadhi) hutegemea majibu ya mitandaoni, kwa kigezo cha kujifunza zaidi (hapa yaweza kuiwa kweli ama uvivu wao wa kufikiri tu, ama siyo kweli). Mwl anatoa homework, mtoto anaenda kumuuliza mzazi ama mlezi wake, mlezi/mzazi huyo anagoogle tu, anampa majibu, kesho yake mwalimu naye kumbe jana yake aligoogle, anampasisha, ikija NECTA wanaivizia Div 5 (kwa wale wa sekondari). Fuatilieni sana shule za Academic, homework wanazopewa watoto wenu na mlinganishe majibu yao kama yapo tofauti na ya google.
Nami ni mtazamo wangu huo.

Ahsante!
 
Naamini watajitetea sana walimu (baadhi), ama wale wa shule za Academic, fuatilieni tena narudia watoto wenu wanaosoma huko, mtoto anakaririshwa kuhesabu 1-10 kwa kiingereza, unamuuliza baadaye, haya hesabu sasa kwa kiswahili, anaanza kujibalaguza hapo, yaani hajui ama hawezi, akirudi nyumbani, tena kukiwa na wageni (hii wanayo sana wanawake, sorry lakini), wanaulizwa 'haya hebu hesabu hadi ten (awasemi kumi)', mtoto anaanza one, two, three,,, na kuendelea, hapo mzazi furaha tele, ila mgeni akikosea akamuuliza mtoto, haya tuhesabie kwa kiswahili, mzazi / mlezi anatoa macho kweeeli.
Tuacheni hizo jamani, tusaidie kwa pamoja kuithamini lugha yetu, tuwasaidie watoto wetu kujenga uwezo wa kujiamini binafsi, hasa kufikiri kwa kina, kuanzia kwetu wazazi hadi waalimu - naamini mpo waalimu humu, tena wengi kweli.

N:B

Siyo academic school zote zinazkaririsha watoto, nimetaja academic ili ujumbe ufike kwa urahisi, zipo hata kayumba shule zinakaririsha watoto, hasa kama kuna walimu wa kugoogle hapo.

Asante kwa kusoma. Na maoni yako.
 
Asante kwa maoni mazuri.
 
"Yeyote ambaye anakubali Mawazo ya wengine bila kuyachuja huyo alipewa ubongo kwa makosa, kwake uti wa mgongo ungemtosha" Nime-paraphrase maneno ya Albert Einstein
^^
 
Umenikumbusha kuna siku nilifanya jaribio kuuliza swali flani la ajabu Google sikupata jibu
 
Back
Top Bottom