"Unataka kuwa nani ukiwa mkubwa?" Hili swali halikuwa Fair kwetu watoto wa Uswahilini

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Tukiacha wale waliokulia kwenye exposure na kila kitu, Uswahilini au mitaani ambapo wengi tumekulia tulikuwa hatunaexposure ya vitu vingi sana. Kuna watu hadi wanafika Chuo kikuu walishataka kuwa karibu kila kitu na hajui kwa nini na ni lini waliamua kusoma hicho wanachosoma..

Ukiwauliza watoto wengi watasema, kulingana na kile wanachokiona au walichokisikia. Hii inamsababisha mtoto kukua akiwa na picha hafifu ya uhalisia wa mambo.
Mfano; aliyezoezwa kuangalia movie, atakwambia nataka kuwa Stering au wengi watasema nataka Kuwa kama Baba bila kujali baba anafanya nini.

Nini kifanyike.
Watoto wetu tuwatembeze sehemu nyingi, Tuwafunulie mambo mengi yenye maana wakiwa wadogo, Kama unaweza unapanga safari kumtembeza kwenye Maonyesho,Jeshini,Bandarini,Ikulu nje ya fensi pale, Makongamano na exhibitions, Mashamba makubwa ya kibiashara, Wafugaji wakubwa, Viwandani, Bungeni, Airport,Mbugani,Migodini, Nenda nae kwenye mijadala ya kujenga,Bila kujali gharama Unaweza kwenda hata nchi yoyote EA ajionee wengine wanaishije. ETC

Unakumbuka Ulivyokuwa mtoto, Ulitamani kuwa nani...
 
mm nilipokua dogo teacher wa shule ya msingi nilikua na muona ndio hero wangu na hakuna kama yeye ..
na nilikua nastruggle ili angalau nimkaribie yeye,.
maana nilikua naona kumzidi haiwezekani
 
mm nilipokua dogo teacher wa shule ya msingi nilikua na muona ndio hero wangu na hakuna kama yeye ..
na nilikua nastruggle ili angalau nimkaribie yeye,.
maana nilikua naona kumzidi haiwezekani
Waalimu ndio watu wa karibu kuwaona kuwa majembe kuliko mtu yoyote duniani.
Hasa mwalimu wa hesabu alafu akiwa mwanamke, shule ya msingi...
 
nilitaka kuwa pilot Mara saa zingine niseme mjeshi
Ila nilivyokuwa Mkubwa nimejikuta napenda sana mambo ya it na ukicheki computer zenyewe tumezijulia ukubwani
 
Back
Top Bottom