mourisous
JF-Expert Member
- Jan 19, 2016
- 443
- 269
UNATAKA ULIMWENGU UKUPENDE KWANI UNATAKA KUUBEBEA MIMBA?
Umeingia kwenye ndoa na mwanaume unayempenda nayeye anakupenda na anakuonyesha mapenzi yote. Lakini hupatani na Mama yake, bila sababu yoyote ile Mama mkwe anakuchukia.
Kuna dada yake kwa maana ya wifi yako ambaye hamuongei kabisa, hujui kwanini kwani hujamfanyia chochote kibaya lakini hamuongei kabisa, shemeji yako mabaye kila siku ni kukutukana!
Kuna rafiki zake ambao unahisi kama wamnakudharau, unawaona kabisa wananuna kila mkiongozana na mume wako. Hapo unaanza kupaniki, unaanza kusema kuwa hupendwi, mbali na kulalamika lakini unaanza kujipendekeza.
Unajipendekeza kwa Mama mkwe, kwa wifi zako na marafiki zake, lakini haisaidii kwani ndiyo kwanza wanazidi kukuchukia, hakuna zuri hata moja ambalo unalifanya wanaliona kama zuri, kila kitu kwao wanakiona kibaya, unapaniki zaidi.
Unajua nini kinatokea Dada yangu, unajikuta unashindwa kuona upendo anaokuonyesha mume wako eti kwakua ndugu zake hawakupendi.
Ndani huna amani kila siku ni kumlalamikia mumeo kuwa wifi kanifanyia hiki, Mama kanifanyia kile, sijui mdogo wako hivi shemeji vile na vile.
Ndiyo mume akirudi nyumbani badala ya kupumzika, muongee kuhusu siku zenu zilikuaje, kuhusu watoto wenu mtawaleaje mnaishia kuongea kuhusu ndugu zake wamakufanyiaje.
Badala mume afaidi chakula kitamu ulichompikia, afaidi mwili wako mtamu unaanza kumsimulia stori za Dada yake ambaye tangu udogo nao walikua hawapatani, stori za Mama yake ambaye naye ashamchoka sema anamvumilia kwakua ni Mama yake atafanyaje?
Unajua nini kinatokea? Mume anachoka malalamiko yako, kila siku anakuambia achana nao lakini “Samahani nataukana kidogo ili inoge” Pumbavu husikii wewe ni kulalamika tu!
Unalalamika unafikiri umeolewa na Mama mkwe, unafikiri unalishwa na marafiki zake, unafikiri wifi zako ndiyo wanakutandikia kitanda! Mume anachoka, hataki hata kurudi nyumbani kwani umekua kero kila siku kulalamika.
Mara nayeye anaanza kukuchoka, mara nayeye anaona mapungufu yako, upendo unapungua anakua hana amani anatafuta sehemu ya kupata amani halafu unaendelea kulia hupendwi huna bahati sijui nini!
Narudia tena, acha ujinga, unataka upendwe na watu wote wewe umekua nani? Mungu mwenyewe na kutuumba yeye lakini hapendwi na watu wote, hata Malaika aliowamumba hawakumpenda wote sembuse wewe!
Dada yangu ukipendwa na mumeo inatosha kabisa, mtu ambaye huamki naye kitanda kimoja anakuhusu nini kama akikuchukia. Mama mkwe akupende kwani unamfikisha kileleni, aache kumpenda mumewe na wanae akupende wewe!
Nikuambie kitu, hembu acha kulalamika kuwa ndugu hawakupendi, waambie kabisa kuwa upendo wa mumeo unakutosha. Majirani wakupende kwani unawalipia kodi za nyumba! Waache kupenda watoto wao waje kukupenda wewe ambaye hata jina hawakujui vizuri.
Hembu acha huo ujinga wa kujaribu kuridhisha kila mtu, mumeo akiridhika inatosha hao wengine nao wakatafute watu wa kuwaridhisha.
Nimechoka kuandika sasa wewe endelea kulalamika kila siku kuwa Mama mkwe hakuipendi kana kwamba unataka umebee mimba huyo Mama mkwe, akupende kwani yeye ndiyo alikutongoza!
Kama unajiamini vyakutosha basi wewe share tu ujumbe huu, lakini kama ni wale ambao mnataka kupendwa na ulimwengu basi endelea kulia lia kuwa hupendwi! Upendwe na kila mtu umekua pesa wewe! Peda pekee ndiyo inapendwa na kila mtu!